Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu wa UN António Guterres akihutubia ufunguzi wa mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la UN
UN /Cia Pak

Tunahitaji ubia wa dunia wakati huu ambao mgawanyiko unazidi- Guterres

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu Antonio Guterres amezungumza wakati wa ufunguzi akigusia masuala lukiki ikiwemo mgawanyiko wa kisiasa na kijiografia duniani, mizozo, uhaba wa chakula, ongezeko la gharama ya maisha, mabadiliko ya tabianchi na teknolojia akisema maendeleo yaliyofikiwa katika Nyanja mbali mbali yanakwamishwa na mgawanyiko wa kisiasa na kijiografia.

Emmanuel Cosmas Msoka, Mchechemuzi wa Vijana wa UNICEF Tanzania kuhusu usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu.
UN/Anold Kayanda

Maneno ni bei nafuu sana lakini vitendo ni bei ghali, tushirikishe vijana kwa vitendo:Msoka  

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu leo unakunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani. Mkutano huo wa siku tatu umeitishwa ili kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya elimu hasa kwa kuzingatia suala la usawa na ujumuishwaji, ubora wa elimu na umuhimu.  

Sauti
2'23"
Taswira wa darasa la mfano linalolenga kuonesha Mgogoro wa kujifunza duniani. Darasa hili lililoandaliwa na UNICEF liko makao makuu ya UN jijini New York, Marekani.
© UNICEF/Chris Farber

Mtoto 1 kati ya 3 duniani kote ndiye awezaye kusoma na kuelewa hadithi fupi na hali si shwari - UNICEF

Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani ukianza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa taarifa inayoeleza idadi ya Watoto wasiojua kusoma imeongezeka ulimwenguni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita. 

Audio Duration
2'31"
Kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan inayoonekana kutoka juu ina wakimbizi kutoka Syria.
UN Photo/Mark Garten)

Watoto wangu wananiuliza Syria ni nini? Kambi ya Zaatar ikiingia muongo mwingine

Mwaka 2022 ni  miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan, kambi ambayo inasimamiwa na Umoja wa Mataifa. Ni kambi kubwa zaidi Mashariki ya Kati na moja ya kambi kubwa zaidi duniani ikiwa ni maskani ya wasyria 80,000. UN News au Habari za UN imezungumza na baadhi ya wakimbizi kuhusu maisha katika kambi hiyo, na matumaini yao kwa siku zijazo. 

Waathirika wa mafuriko kwenye eneo la Balochistan, nchini Pakistani.
WFP Pakistan

Msifurishe dunia hii leo, wala msiizamishe kesho- Ujumbe wa Katibu Mkuu wa viongozi wa dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani hii leo ikiwa ni kuelekea Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN unaoanza wiki ijayo akisema ujumbe wake mkuu kwa viongozi watakaoshiriki ni dhahiri ya kwamba wachukue hatua kupunguza kiwango cha joto duniani.

Sauti
3'45"
Sidonie, mwenye umri wa miaka 10, akiwa mbele ya darasa la shule yake ya msingi Kitambo iliyoko mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Kinshasa.
© UNICEF/Josue Mulala

Elimu ya sasa inapitia janga kubwa: Tuirekebishe kwa mustakabali wa watoto

Ingawa msemo wa haki ya binadamu umezoelekea, hakuna haki ya binadamu yoyote ambayo imetolewa bure bila kupiganiwa, vivyo hivyo inapaswa kuwa kwa elimu, amesema Leonardo Garnier, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani, mkutano unaoanza Ijumaa hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kufahamu msingi wa kauli hiyo, 

Sauti
2'
Tarehe 16 mwezi Juni mwaka 2022 mtoto wa kike akitumia pampu ya mkono kupata maji kutoka bwawa la mchanga lililojengwa na UNICEF huko Kanyangapus kaunti ya Tukrana nchini Kenya.
© UNICEF/Paul Kidero

Mabwawa ya mchanga Turkana yaepusha wanawake kutembea kilometa 10 kusaka maji

Katika Kijiji cha Kanyangapus Kaunti ya Turkana nchini Kenya hali ya ukame ni mbaya sana kila kona na moja ya athari kubwa zilizoambatana nao ni ukosefu wa maji.  Mabwawa ya mchanga yamekuwa suluhu bunifu inayozisaidia kaunti nyingi zilizo katika hali ya nusu jangwa nchini Kenya na shukrani kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kufadhili wa mradi huo wa ujenzi wa mabwawa ya mchanga na pampu za maji, sasa adha ya maji katika kaunti ya Turkana imepungua na hususan kwa wanawake wanaolazimika kwenda umbali mrefu kusaka maji. 

Sauti
2'40"
Katibu Mkuu Antonio Guterres akipanda meli ya Kubrosliy huko Odesa, Ukraine.
UN Photo/Mark Garten

Kila meli inayoondoka Odesa imebeba matumaini- Guterres

Leo hii Odesa ni zaidi ya bandari ya kusafirisha, shehena, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo alipotembelea bandari hiyo iliyoko Ukraine, kujionea upakiaji wa shehena za nafaka na chakula kufuatia makubaliano ya kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi, makubaliano yaliyowezesha kuanza kusafirishwa kwa bidhaa hizo kwenda soko la dunia licha ya uvamizi unaoendelea wa Urusi nchini Ukraine.