Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 60 ya mkataba wa kutokuwa na utaifa tumepiga hatua:Grandi

Watoto katika kambi ya watu walioyakimbia makazi yao nchini Nigeria walionesha yeti vyao vya kuzaliwa, nyaraka muhimu ya kuonesha utaifa wao
© UNHCR/Gabriel Adeyemo
Watoto katika kambi ya watu walioyakimbia makazi yao nchini Nigeria walionesha yeti vyao vya kuzaliwa, nyaraka muhimu ya kuonesha utaifa wao

Miaka 60 ya mkataba wa kutokuwa na utaifa tumepiga hatua:Grandi

Masuala ya UM

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokuwa na utaifa, mkataba wa kukabiliana na tatizo hilo unaadhimisha miaka 60 ya kukuza na kulinda haki za watu wasio na utaifa . 

Katika ujumbe wake wa siku hii Kamisha mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi amesema leongo kubwa la mkataba huo uliotiwa Saini na kupitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1961 ni kuhakikisha haki ya utaifa na kutokomeza kabisa hali ya kutokuwa na utaifa kunapatikana na ni jambo la muhimu zaidi sasa kuliko hapo awali. 

"Changamoto mpya za ulimwengu, kama vile COVID-19 na athari za mabadilikoya tabianchi, juu ya zile zinazoendelea kama kuongezeka kwa watu kufuriushwa katika makazi yao, zinaonyesha jinsi gani haki ya utaifa ilivyo muhimu. Kila mtu anahitaji kuhesabiwa na kuonekana machoni pa nchi yake na serikali, na kujumuishwa katika hatua za kukabiliana na tatizo hilo,"amesema Grandi. 

Ameongheza kwamba "Kuwa na utaifa na ulinzi wa serikali ambayo utaifa unatolewa kunaweza kuleta mabadiliko ya kuokoa maisha, hasa zaidi wakati wa shida, iwe ni chanjo, uokoaji au hifadhi ya mfuko wa kijamii ambao unahitajika,"

UNHCR inasema watu wasio na utaifa wanaweza kutumbukia katika majanga kwenye hali ya mizozo kwa sababu wanakosa ulinzi wa serikali yoyote, hawana uthibitisho wa kitambulisho chao cha kisheria, au vyote viwili.  

Wana hatari pia ya kutengwa katika masuala ya kupata chanjo za COVID-19 wakati nchi zinatekeleza mipango ya kukabiliana na janga hilo.

Vivyo hivyo, jamii zisizo na utaifa hazina uwezekano wa kujumuishwa katika vifurushi vya misaada ya kijamii na kiuchumi iliyokusudiwa kupunguza athari za janga hilo kwa maisha ya watu.  

Shirika hilo la wakimbizi limeongeza kusema, wakati mabadiliko ya hali yatabianchi yanazidi kuwa mbaya, watu wasio na utaifa wana hatari ya kutengwa na juhudi za serikali za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Mkimbizi w andani nchini Niheria akifurahi kuwa mtoto aliyejifungua atapata cheti cha kuzaliwa
© UNHCR/Gabriel Adeyemo
Mkimbizi w andani nchini Niheria akifurahi kuwa mtoto aliyejifungua atapata cheti cha kuzaliwa


  Kukosa utaifa ni kukosa huduma 
 

Bwana Grandi amesema kimsingi “Kutokuwa na nchi au utaifa kunaweza kumaanisha kutokuwa na ufikiaji  wa huduma za msingi kama elimu, matibabu au ajira za kisheria. Ukosefu wautaifa unaweza kuzuia uhuru wa kutembea, uwezo wa kununua mali, kupiga kura, kufungua akaunti ya benki au hata kuoa. Ulimwenguni, watu milioni 4.2 wanajulikana kuwa hawana utaifa. Lakini, idadi ya kweli ya watu ambao hawatambuliki kama raia na nchi yoyote inaweza kuwa kubwa zaidi, ikizingatiwa mapungufu katika ukusanyaji wa tamwimu”. 
 
Kwa mantiki hiyo amesema “Mkataba wa mwaka 1961 ni mkataba muhimu wa kimataifa ilioundwa kuzuia na kupunguza ukosefu wa utaifa. Ikiwa unatumiwa na Mataifa yote, utasaidia kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayezaliwa bila utaifa na hatimaye utasaidia kutokomeza tatizo la muda mrefu la kutokuwa na utaifa.” 
Kufikia mwisho wa Agosti 2021, Mataifa 77 yamejiunga na Mkataba wa 1961, huku idadi ikiongezeka kwa kasi katika muongo mmoja uliopita.  
Tangu mwaka 2010, Mataifa 40 yamerasimisha ahadi zao za kupunguza tatizo la ukosefu wa utaifa kwa idadi kubwa ya watu kwa kuwa wanachama wa mkataba huo na nchi zilizojiunga hivi karibuni kabisa ni Iceland na Togo. 

Katika kipindi hicho hicho, zaidi ya watu 800,000 wasio na utaifa sasa sasa wamethibitishwa kupata utaifa na tatizo lao kutatuliwa. 
"Katika maadhimisho ya mwaka huu, UNHCR inahimiza mataifa yote ambayo hayajafanya hivyo kujiunga na mkataba wa 1961 wa kupunguza tatizo la kutokuwa na utaifa, kuingiza kinga za mkataba katika sheria zao za utaifa, na kuhakikisha haki ya kila mtu ya utaifa, ”amesema Grandi. 

Kujiunga na mkataba wa 1961 ni moja wapo ya hatua 10 za mpango wa utekelezaji wa kimataifa wa kukomesha ukosefu wa utaifa.  
Mpango huo unatoa mfumo kwa mataifa kufikia malengo ya kampeni ya #IBelong, ambayo ilizinduliwa na UNHCR na washirika wake mnamo 2014 kumaliza tatizo la kutokuwa na utaifa ndani ya miaka 10.