Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kwanza wa vifaa tiba wawasili Afghanistan:WHO 

Mhudumu wa afya akihudhumia mvulana jimbo la Parwan nchini Afghanistan, Novemba 2020.
© WFP/Massoud Hossaini
Mhudumu wa afya akihudhumia mvulana jimbo la Parwan nchini Afghanistan, Novemba 2020.

Msaada wa kwanza wa vifaa tiba wawasili Afghanistan:WHO 

Afya

Ndege iliyobeba dawa na vifaa vya vingine vya afya vya kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO imewasili Afghanistan leo, 30 Agosti, majira ya jioni kwa saa za nchi hiyo. 

Hii ni safari ya kwanza ya vifaa vya matibabu kuwasili nchini Afghanistan tangu nchi hiyo ilipodhibitiwa na mamlaka ya Taliban takribani wiki mbili sasa. 

"Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila kukoma ili kupata suluhisho, ninafurahi kusema kwamba sasa tumeweza kujaza sehemu ya akiba ya vituo vya afya nchini Afghanistan na kuhakikisha kuwa kwa sasa huduma za afya zinazoungwa mkono na WHO zinaweza kuendelea," Amesema Dkt. Ahmed Al Mandhari, mkurugenzi wa kikanda wa WHO kwa eneo la Mediterania ya Mashariki. 

WHO inasema tani 12.5 za vifaa tiba vilivyowasili ni pamoja na vifaa vya hudumia wenye kiwewe na vifaa vya afya vya dharura, na vinatosha kushughulikia mahitaji ya msingi ya afya ya zaidi ya watu 200 000, pia kutoa taratibu humuma 3,500 za upasuaji na kutibu wagonjwa wa wenye kiwewe 6,500. 

Vifaa tiba hivyo vitapelekwa mara moja kwenye vituo 40 vya afya katika majimbo 29 kote nchini Afghanistan. 

Ndege nyingine zaidi za vifaa kufuata 

Ndege hiyo, ambayo ilitolewa na Serikali ya Pakistan, ilipakiwa vifaa mapema leo na timu ya vifaa ya WHO katika jiji la kimataifa lenye ghala la mahitaji ya kibinadamu huko Dubai, katika nchi za Falme za Kiarabu, na ikapita moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa Mazar-i-Sharif nchini Afghanistan. 

Hii ni ndege ya kwanza kati ya ndege tatu zilizopangwa na Shirika la ndege la Pakistan (PIA) kusaidia kuziba pengo la upungufu wa dawa na vifaa vya matibabu nchini Afghanistan. 

“Ningependa kuishukuru Serikali ya Pakistan na shirika la Ndege PIA kwa juhudi zao za kusaidia WHO na watu wa Afghanistan. Mashirika ya kibinadamu kama vile WHO yamekabiliwa na changamoto kubwa katika kutuma vifaa vya kuokoa maisha kwa Afghanistan katika wiki za hivi karibuni kutokana na vikwazo vya usalama na vifaa. Msaada wa watu wa Pakistani umekuwa wa wakati unaofaa na wa kuokoa maisha,”ameongeza Dkt Al-Mandhari. 

WHO inafanya kazi na washirika wengine kuhakikisha kuwa usafirishaji wa wiki hii ni wa kwanza kati yausafirishaji mwingine mwingi utakaofuata.  

Daraja la kuaminika la usafirishaji misaada ya kibinadamu linahitajika haraka ili kuongeza juhudi za pamoja za kibinadamu. 

Umakini wa dunia kwa wiki 2 zilizopita umejikita zaidi na uokoaji wa maisha kwa kusafirisha misaada kwa njia ya angana kuwahamisha watu waliokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Kabul.  

Sasa WHO imesema kazi iliyovabi ya kibinadamu ya kukidhi mahitaji ya mamilioni ya Waafghan walio katika mazingira magumu ambao wanasalia nchini Afghanistan ndio sasa inaanza, dunia haiwezi kuwapa kisogo watu wa Afghanistan wakati huu muhimu.