Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka jukumu moja la kupinga ubaguzi wa rangi hadi jingine : Andrew Young anavyomkumbuka Ralph Bunche

Ralph Bunche ( Mmarekani 1904 - 1971) Afisa wa Umoja wa Mataifa, Msindi wa tuzo ya Amani ya Nobel
UN Photo.
Ralph Bunche ( Mmarekani 1904 - 1971) Afisa wa Umoja wa Mataifa, Msindi wa tuzo ya Amani ya Nobel

Kutoka jukumu moja la kupinga ubaguzi wa rangi hadi jingine : Andrew Young anavyomkumbuka Ralph Bunche

Masuala ya UM

Andrew Young, Balozi wa kwanza wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa mwenye asili ya Afrika akiwa anaandika historia hiyo amem mwagia sifa Ralph Bunche kuwa mtu aliyekuwa akimvutia

Bunche, aliyefariki dunia miaka 50 iliyopita, alikuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrika kushinda tuzo ya amani ya Nobel na alikuwa na jukumu kubwa katika siku za mwanzo za Umoja wa Mataifa.

Katika mazungumzo yake na idara ya habari ya Umoja wa Mataifa July 2020 Andrew Young alieleza kwanini ushawishi wa Bunche unaendelea kuonekana mpaka leo katika harakati za uwanda mpana wa kupiga vita ubaguzi. 

Ralph Bunche alikuwa mmoja wa mashujaa wangu wautotoni. Nilikuwa namuona kama baba yangu, kwasababu alikuwa ameshafanya kila kitu nilichokuwa najaribu kufanya miaka 40 kabla.

Ralph aliacha chuo kikuu cha Howard (mmoja ya vyuo vikuu maarufu vyenye historia ya watu Weusi) mwaka 1939 na kufanya ziara barani Afrika, kuunda intelijensia ya kijeshi barani humo kwenye mapambano ya vita ya pili ya dunia kwa ajili ya Marekani.

Alizunguka na boti katika nchi za Morocco, Tunisia na Misri na kisha kupitia mfereji wa Suez kwenda nchini Kenya na Afrika Kusini, na alikuwa mtu pekee kwenye jeshi la Marekani aliyekuwa akijua kitu kuhusu bara la Afrika, katika nyanja ya kiintelijensia au masuala ya ujasusi

Mafundisho mengi ya Umoja wa Mataifa, yale ya kupinga utumwa, ulinzi wa amani, na uhamiaji, wakimbizi, kuomba hifadhi, yalikuja naamini kutoka kwa wanafunzi aliowafundisha katika kipindi chake. 

Balozi Andrew Young wa Marekani, Rais wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, akiwa ameitisha mkutano wa kuijadili nchi ya Afrika Kusini ( Machi 1977)
UN Photo/Yutaka Nagata
Balozi Andrew Young wa Marekani, Rais wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, akiwa ameitisha mkutano wa kuijadili nchi ya Afrika Kusini ( Machi 1977)

 Raia wa Marekani aliyeandamana kwa ajili ya uhuru

Wakati wa vuguvugu la kudai haki za uraia, na ingawa alikuwa afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa  na hakuhusika moja anahusika moja kwa moja na Martin Luther King , hakusita kumshauri na kumtia moyo Dkt. King.

Na hata alikuja na kuandamana pamoja na Dkt.King huko Selma (Maandamano ya mwaka 1965 yasiyo ya vurugu ya wanaharakati, kuonesha ukandamizwaji wa haki yao ya kupiga kura ya kikatiba) akionesha hatakama ni msomi mashuhuri wa kimataifa, alikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na jamii ya watu weusi na viongozi wa wanaodai haki za raia: hakuja kama afisa wa Umoja wa Mataifa, alitaka kuwapo eneo hilo kama raia wa Marekani, akiandamana kupata uhuru katika nchi yake.

Nilipokutana na Bwana Bunche kwenye Umoja wa Mataifa [mnamo mwaka 1967, nikimsindikiza Martin Luther King] alisema kwamba hataki kumkosoa Dk King kwa msimamo wake juu ya Vietnam, ambayo alikubaliana nae [Martin Luther King alikuwa akipinga vikali kuhusu Marekani kushiriki katika vita vya Vietnam], lakini alisema kwamba alichukia kuona Dk King akihusika katika harakati zote za kudai haki za raia na kudai haki kwa amani wakati huo huo kwani zilikuwa zikimuacha wazi sana.

Dk King alijibu kwamba hakutaka kuhusika katika masuala yote mawili lakini hakuwa na chaguo: "Sitaki kuhusika na hii, lakini siwezi kulikimbia. Siwezi kutenganisha ufahamu wangu. Siwezi kuwa upande wa wasiotaka vurugu, kati ya jamii na matabaka ya ulimwengu na kuidhinisha vurugu katika mizozo ya kimataifa ".

Mkutano huo ulifanyika mwaka mmoja na siku moja kabla ya Dk King kuuawa. Ni kana kwamba Bunche alikuwa akitabiri kuwa majukumu aambayo Dr King alikuwa akichefa hayakuwa ya busara, na alikuwa akimshauri apunguze kidogo ili aweze kudumu kwa muda mrefu.

Dkt. Martin Luther King na mke wake Coretta Scott King wakionekana wakiwa wanasalimiana na Ralph J. Bunche, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya kisiasa.  Mr.Bunche alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1950
UN Photo/Yutaka Nagata
Dkt. Martin Luther King na mke wake Coretta Scott King wakionekana wakiwa wanasalimiana na Ralph J. Bunche, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya kisiasa. Mr.Bunche alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1950

 Mtaalamu wa usuluhisi kupitia milango ya nyuma

Ralph Bunche kila wakati alikuwa na busara na mantiki, na alipinga kila aina ya siasa za kihemko na hasira ambazo zingeweza kuwepo miongoni mwa jamii, au kati ya nchi zilizo endelea na zinazoendelea.

Alikuwa mpatanishi mkuu, mwenye akili na kufanya mambo kimantiki, na kwa uchambuzi, ambao aliutumia kwa masuala na yenye mihemko. Hakuamini kwenye usiri, lakini aliamini kuwa diplomasia inategemea kiwango fulani cha ujasiri wa kibinafsi: kuna mchezo unaendelea nyuma ya pazia siku zote katika Umoja wa Mataifa.

Nakala hii ni moja ya mfululizo wa Makala za kuadhimisha miaka 20 ya Azimo la Durban la Umoja wa Mataifa, linalochukuliwa kuwa moja ya hatua muhimu katika vita vya ulimwengu dhidi ya ubaguzi wa rangi. 

Msuluhishi wa Palestina, Dkt Ralph Bunche ( Kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tyve Lie
UN Photo/MB
Msuluhishi wa Palestina, Dkt Ralph Bunche ( Kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tyve Lie

 Ralph Bunche, mpenda amani

Mafanikio ya  Ralph Bunche nivigumu kutozungumziwa. Wakati wa kutangazwa kwa ubaguzi wa rangi nchini Marekani Bunche alikua Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kupata udaktari kutoka chuo kikuu cha Marekani mwaka 1930. Baada ya kuitumikia nchi yake katika Vita ya pili ya dunia, katika ujasusi wa kijeshi, alifanya kazi kwenye hati mbili zamsingi za Umoja wa Mataifa. (Katiba ya Umoja wa Mataifa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu)

Bwana Bunche aliendelea kufanya kazi Umoja wa Mataifa mpaka kufikia ngazi ya Msaidizi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akiunga mkono juhudi za watu waliokaliwa na wakoloni kupata uhuru na uhuru katika Baraza la Udhamini, Trusteeship Council, na kuwa mpatanishi mwaka 1949 kati ya Israeli na nchi jirani za Kiarabu, ambapo alipewa tuzo ya Amani ya Nobel mnamo  mwaka 1950. 

Bwana Bunche alikuwa miongoni wa waliobuni na kusimamia utekelezaji wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, na yeye mwenyewe aliongoza kubwa na yenye changamoto kubwa kati ya hizo, operesheni ya Umoja wa Mataifa ya mwaka  1960 nchini Jamuhuri ya Kidemokraisa Kongo DRC.