Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Shirika la chakula duniani, WFP likisambaza mgao wa chakula katika jimbo la Ituri, DRC. (21 Machi 2018.)
WFP/Jacques David

WFP inahitaji kuongezewa nguvu ili kupambana na Ebola.

Wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC ikipambana na mlipuko wa pili mkubwa wa ugonjwa wa Ebola, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limetahadharisha hii leo mjini Goma kuwa rasilimali zinazohitajika kusaidia shughuli zake, haziendani na kasi ya ongezeko la hivi karibuni la maambukizi na uwepo wa hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo ndani ya DRC na katika nchi za jirani.

María Fernanda Espinosa Garcés;Rais wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza hilo
Picha na UN/Cia Pak

Kwa wananchi wa kawaida vitendo ni bora kuliko maneno au hotuba:Espinosa

Maneno matupu na hotuba bila vitendo halisi na hatua zinazoonekana katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu, havina faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Hayo yamesemwa leo na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa ufunguzi wa hafla ya maadhimisho ya kwanza ya siku ya ushirikiano wa kimataifa na amani kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New york Marekani.

WFP yaanzisha mpango wa msaada wa chakula kwa watu walioathirika na Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
WFP/Olivier Nkakudulu

Tuongezeeni nguvu ili tukabiliane vyema na Ebola DRC- WFP

Wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC ikipambana na mlipuko wa Ebola ambao ni wa pili kwa ukubwa katika historia ya nchi hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limetahadharisha hii leo mjini Goma kuwa rasilimali zinazohitajika kusaidia shughuli zake, haziendani na kasi ya ongezeko la hivi karibuni la maambukizi na uwepo wa hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo ndani ya DRC na katika nchi za jirani.

 Ufunguzu wa  mkutano wa Mataifa ulifanyika Geneva tarehe 15 Novemba 1920
UN Photo/Jullien

Ushirikiano wa kimataifa ni nguzo kwa dunia na kila mmoja:Guterres

Ushirikiano wa kimataifa na diplomasia vimethibitisha kuwa na faida na huduma muhimu kwa watu wote duniani kuanzia masuala ya utekelezaji wa sheria za kimataifa, usawa wa kijinsia, ulinzi wa mazingira, hadi kuzuia uzalishaji wa silaha za maangamizi na hata magonjwa hatari duniani, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa maadhimisho ya kwanza ya kimataifa hii leo ya “siku ya ushirikiano wa kimataifa na diplomasia kwa ajili ya amani”