Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

BU linakutana kushauriana juu ya Burundi, Usomali na JKK

Baraza la Usalama leo asubihi linazingatia hali katika Burundi kwenye kikao cha hadhara. Baada ya hapo Baraza litasailia kazi za Kamati ya Vikwazo dhidi ya JKK (DRC). Alasiri Baraza la Usalama linatarajiwa kuwa na mashauriano maalumu kuhusu maendeleo katika juhudi za kimataifa za kurudisha usalama na amani nchini Usomali, kikao ambacho pia kitahudhuriwa na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah.~

Misaada ya kiutu ina ugumu kufikishwa Ossetia Kusini, inasema OCHA

Mashirika mbalimbali ya UM yamethibitisha kwamba shughuli za kupeleka misaada ya kiutu katika Ossetia Kusini, kwa kupitia Georgia yenyewe, bado haziwezekani kuhudumiwa kwa sababu ya ukosefu wa maafikiano kati ya makundi yanayohasimiana kuruhusu misaada hiyo kufikishwa,bila vizingiti, katika Ossetia Kusini kwa kutumia barabara za Georgia. Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) aliwadokezea waandishi habari mjini Geneva juu ya tatizo hili:~

Hapa na pale

Taarifa kwa waandishi habari iliotolewa Ijumanne (26/08/2008) na Shirika la Mchanganyiko la UM/UA Kulinda Amani Darfur (UNAMID) kuhusu mashambulio ya kambi ya wahamiaji wa ndani (IDPs) ya Kalma, iliopo katika jimbo la magharibi la Sudan, ilishtumu, kwa lugha ya uzito mkuu, kitendo cha kutumia mabavu ya kuua yaliokiuka mipaka na yasiowiana kilichoendelezwa na vikosi vya usalama vya Serikali ya Sudan dhidi ya raia, kitendo ambacho UNAMID ilisisitiza kilitengua haki za kimsingi na kusababisha ajali mbaya ya vifo na majeruhi kwa wakazi katika kambi hiyo.

UM washiriki kwenye mkutano wa Afrika kupiga vita ubaguzi wa rangi

Kuanzia Ijumapili tarehe 24 Agosti (2008) maofisa wa UM pamoja na wawakilishi wa serikali za Afrika na wataalamu kutoka jumuiya za kiraia, hali kadhalika, walikutana kwenye mji mkuu wa Abuja, Nigeria kwenye kikao cha siku tatu, kuzingatia masuala yanayohusu ukabila, ubaguzi wa rangi, chuki za wageni na mifumo mengineyo inayofungamana na utovu wa kustahamiliana.

Guineau-Bissau ni mwenyeji wa mkutano wa UM kuzingatia hali Afrika Magharibi

Mkutano wa kiwango cha juu wa siku mbili, unaohudhuriwa na Wajumbe Maalumu wa KM pamoja na wakuu wa mashirika yanayosimamia operesheni za ulinzi wa amani Afrika Magharibi, leo umeanzisha majadiliano katika Guinea-Bissau ambapo kunafanyika tathmini mpya juu ya hali, kijumla, na kusailia, hususan, taratibu za chaguzi zijazo katika mataifa ya Cote d’Ivoire, Guinea-Bissau na katika Jamhuri ya Guinea, vile vile kuzingatia udhibiti bora wa mipaka kwa sababu ya fununu za karibuni kwamba eneo la Afrika Magharibi siku hizi hutumiwa kusafirishia magendo ya madawa ya kulevya.

Wajumbe wa Afrika wanashirikiana na UM Addis Ababa kuzingatia maendeleo ya wanawake

Darzeni za wataalamu wa kutoka Wizara za Masuala ya Kijinsia na Maendeleo ya Wanawake wakijumuika pamoja na wawakilishi wa makundi ya kieneo na kutoka mashirika ya UM, na vile vile waandishi habari, wamekusanyika hii leo Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria mkutano wa siku mbili, ulioandaliwa bia na UM/UA, kusailia maendeleo ya wanawake, kijumla, na usawa wa kijinsia katika bara la Afrika. Majadiliano haya yatalenga zaidi juuya utekelezaji wa Sera za Kijinsiya za UA, mradi ambao unahitajia kutekelezwa na mataifa husika kuendeleza usawa wa kijinsiya na maendeleo ya wanawake Afrika.~~~

Hapa na pale

Ameerah Haq, Mshauri Mkazi juu ya Huduma za Kiutu za UM kwa Sudan amesema Umoja wa Mataifa una khofu kuu kuhusu ripoti ilizopokea Ijumatatu asubuhi zenye kuonyesha magari ya polisi wa Sudan yaliizingia kambi ya Kalma, iliopo kilomita 25 kutoka mji wa Nyala, Darfur Kusini ambapo wahamiaji wa ndani (IDPs) wamepatiwa makazi ya muda. Taarifa ziliofuatia zilisema kambi ya Kalma ilishambuliwa baadaye na kusababisha vifo vya raia na majeruhi kadhaa.