UNAMA imethibitisha mauaji ya raia kutoka shambulio la angani katika Herat, Afghanistan
Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afghanistan, Kai Eide, ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la UM la Kusaidia Afghanistan (UNAMA) ametoa taarifa maalumu inayosema UM una “ushahidi hakika wa kuridhisha” wenye kuonyesha raia 90, wakiwemo watoto 60, waliuawa kutokana na shambulio la ndege za Marekani katika jimbo la magharibi la Afghanistan la Heart, wiki iliopita.