Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Usawa wa Kijinsiya Makazini unasisitizwa na ILO

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi Duniani (ILO) limeanzisha kampeni mpya ya kimataifa itakayoendelezwa kwa muda wa mwaka mmoja, iliokusudiwa kuangaza umuhimu wa kuwa na usawa wa kijinsia katika mifumo ya kazi na ajira. Kadhia hii inalingana na mapendekezo ya Ajenda ya Kazi Stahifu, ambayo inajumuisha mada 12 zinazotumiwa kupitia athari za mifumo ya kazi na ajira miongoni mwa wafanyakazi wanaume na wanawake, na kufafanua kama haki zao hutekelezwa kwa usawa. ~~

Wakati umewadia kukomesha kwa vitendo utumiaji mabavu dhidi ya Wanawake

Wiki hii Naibu KM Asha-Rose Migiro alipata fursa ya kuzungumzia suala la udhalilishaji wa kijinsia, kwenye mkutano maalumu uliotayarishwa mjini New York na Halmashauri ya Mataifa ya Ulaya pamoja na Ubalozi wa San Marino katika UM. Kwenye risala alioitoa mbele ya kikao hicho NKM Migiro alihimiza kuchukuliwe hatua za pamoja, kukomesha haraka tabia ya utumiaji nguvu na mabavu dhidi ya wanawake, hatua ambayo ikikamilishwa, alitilia mkazo, itawavua wanawake na mateso hayo maututi.~

Mukhtasari wa Mkutano wa UM Kudhibiti Akiba ya Chakula Duniani

Mkutano Mkuu wa UM kuhusu Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani ulitarajiwa kukamilisha mijadala yake mjini Roma Alkhamisi ya leo na kuwasilisha taarifa ya mwisho ambayo, nilipoelekea studio ilikuwa bado haijapitishwa. Taarifa hiyo ilisubiri uamuzi wa mataifa ya Amerika ya Latina kuhusu matumizi ya nishati inayozalishwa na mavuno ya nafaka, kadhia ambayo hudaiwa ndio inayochochea mifumko ya kupanda kwa kasi bei za chakula na kuongeza athari haribifu katika mazingira.~

UM unaadhimisha Siku ya Kuhifadhi Mazingira Duniani

Tarehe 05 Julai huadhimishwa kila mwaka na jamii ya kimataifa kuwa ni siku ya kukumbushana umuhimu wa hifadhi bora ya mazingira ulimwenguni. Muktadha wa mwaka huu kuiheshimu siku hiyo unatilia mkazo kwa umma wa kimataifa kujiepusha na vitendo vinavyotokana na utumiaji wa nishati yenye kutoa hewa chafu angani, ambayo huharibu mazingira ulimwenguni.

Baraza la Haki za Binadamu linazingatia haki za wanawake

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu aliwaambia wajumbe waliohudhuria majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu (HRC) mjini Geneva, kuzingatia haki za wanawake kwamba bila ya kuwepo sheria za kuwakinga wanawake na mateso, pamoja na utumiaji mabavu dhidi yao, serikali za kimataifa na wote waliodhaminiwa madaraka ya utawala hawatofanikiwa kutekeleza usawa wa kijinsia kuimarisha maendeleo yao:~~

ICC inaishtumu Sudan kwa makosa ya jinai Darfur

Baraza la Usalama limekutana kwenye kikao cha hadhara kuzingatia suala la Darfur. Luis-Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) alitarajiwa kuwakilisha ripoti maalumu yenye tuhuma zinazolenga wenye madaraka Sudan dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu katika Darfur.

Mkutano wa UM Kudhibiti Akiba ya Chakula Duniani waendelea Roma

Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani unaofanyika hivi sasa mjini Roma, Utaliana leo umekamilisha siku ya pili. Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) alinakiliwa akisema “walimwengu wanalazimika, na pia kuwajibika sasa kukamilisha, kwa vitendo, haraka iwezekanavyo, yale mapendekezo ya kukabiliana na tatizo la chakula duniani,” kwa sababu, alionya, “janga la njaa limekakamaa na linaendelea kusonga mbele, kufuatilia mifumko ya bei za chakula na nishati ulimwenguni.”

KM atathminia mzozo wa chakula

KM Ban Ki-moon, kabla ya kuondoka Roma, alikutana na waandishi habari ambapo alinasihi kwamba walimwengu wamekabiliwa na uamuzi mmoja pekee katika kuutatua mgogoro wa chakula duniani. Uamuzi huo ni ule utakaohakikisha tunafanikiwa kulimudu tatizo la chakula kipamoja, ili kuepukana na maafa ya adui njaa.