Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

WaMaasai wa Kenya watasaidiwa na UM kutunza utamaduni wa jadi

Shirika la UM juu ya Hakimiliki za Kitaaluma (WIPO) limeripoti kwamba raia wawili wa KiMaasai wa Laikipia, Kenya wamepatiwa fursa ya kwenda Marekani kushiriki kwenye mafunzo maalumu ya Taasisi ya Kuhifadhi Utamaduni wa Kienyeji, mafunzo ambayo yanatarajiwa kuwapatia ujuzi wa kisasa wa kutunza na kuhifadhi nyaraka za utamaduni wao wa jadi, kwa masilahi ya vizazi vijavyo. ~~

Wahamiaji waliopo Yemen wanaombewa misaada ziada na UNHCR

Kwenye mkutano wa siku mbili uliofanyika kwenye mji wa Sana\'a, Yemen kuzingatia juhudi za kimataifa za kuwapatia hifadhi bora wahamiaji wanaovushwa kimagendo kwenye Ghuba ya Aden kutoka Pembe ya Afrika, kikao ambacho kilikamilisha mijadala yake hii leo, kulitolewa ombi la dharura na Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Antonio Guterres aliyoitaka jumuiya ya kimataifa kuharakisha, na pia kuongeza mchango wao, unaohitajika kuwasaidia wahamiaji hawa kunusuru maisha.

Ban Ki-Moon atazuru maeneo yalioathirika na kimbunga Myanmar

KM Ban Ki-moon atafanya ziara ya siku tatu, kuanzia Ijumatano, katika Myanmar ambapo anatarajiwa kuzuru yale maeneo yalioharibiwa na Kimbunga Nargis, kilichopiga huko mwanzo wa mwezi, hasa kwenye eneo la Delta ya Irrawaddy, sehemu ambayo inasemekana ndio iliothirika sana na tufani hiyo.~~

ASEAN kuanzisha tume ya kuharakisha misaada ya kiutu Myanmar

Wajumbe wa Umoja wa Mataifa ya Kusini-Mashariki ya Asia, yaani Umoja wa ASEAN waliokutana Singapore, leo wameafikiana kuanzisha tume maalumu itakayodhaminiwa madaraka ya kurahisisha ugawaji wa misaada ya dharura, ya kihali, kutoka wafadhili wa kimataifa kwa Myanmar, tume ambayo itaongozwa na KM wa Umoja wa ASEAN, kwa madhumuni ya kuondosha wasiwasi wa wenye mamlaka kuhusu dhamira hasa ya michango ya baadhi ya mataifa ambayo huyatafsiri adui. Tume hiyo inatarajiwa kushirikiana, kwa karibu zaidi, na UM katika kuongoza huduma za kiutu nchini Myanmar.

WHO inawakumbuka waliofariki maafa maumbile Myanmar/Uchina

Kwenye ufunguzi wa kikao cha mwaka cha Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO) mjini Geneva leo Ijumatatu wajumbe wa kimataifa kutoka nchi 193 walijumuika kuwakumbuka watu waliofariki kwenye Kimbunga Nargis nchini Myanmar, na vile vile wale watu walioangamizwa na zilzala iliopiga Uchina majuzi. Wajumbe wa WHO walikaa kimya kwa dakika kuwakumbuka waliokufa.~~