Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-Moon atazuru maeneo yalioathirika na kimbunga Myanmar

Ban Ki-Moon atazuru maeneo yalioathirika na kimbunga Myanmar

KM Ban Ki-moon atafanya ziara ya siku tatu, kuanzia Ijumatano, katika Myanmar ambapo anatarajiwa kuzuru yale maeneo yalioharibiwa na Kimbunga Nargis, kilichopiga huko mwanzo wa mwezi, hasa kwenye eneo la Delta ya Irrawaddy, sehemu ambayo inasemekana ndio iliothirika sana na tufani hiyo.~~

Amanda Pitt, Msemaji wa Ofisi ya OCHA, alikiuwa na mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopo mjini Bangkok, Thailand na aliwapatia fafanizi kuhusu hali halisi ilivyo sasa hivi katika Myanmar.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.