Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi yaliohasimiana yarudia mapigano kwenye eneo la ubishani Sudan

Makundi yaliohasimiana yarudia mapigano kwenye eneo la ubishani Sudan

Makundi yaliohasimiana katika Sudan, yaani majeshi ya Serikali na vikosi vya Sudan kusini, yameripotiwa kurudia tena mapigano yaliofumka, kwa makali yanayoshtusha, kwenye eneo la Abyei, linalopakana kaskazini na kusini ya nchi.