Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

KM ameshtumu mauaji katika Tarafa ya Ghaza

KM Ban Ki-moon ameshtumu upotezaji wa maisha ya raia uliotukia mapema Ijumatatu kwenye Tarafa ya Ghaza, msiba ambao pia ulisababisha vifo kadha, ikijumuisha vifo vya mama mmoja na watoto wake wanne. Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Ofisi ya KM kuhusu tukio hili, vikosi vya Israel vilivyokuwa vikiendeleza operesheni zake katika Ghaza vilikumbushwa tena dhamana walionayo, chini ya sheria za kiutu za kimataifa, ya kuhifadhi na kuwahami raia walionaswa kwenye mazingira ya mapigano.

KM anasailia mgogoro wa chakula na viongozi wa mashirika ya UM

KM Ban Ki-moon ameanza mazungumzo maalumu katika mji wa Bern, Uswiss na wakuu wa mashirika 27 ya kimataifa yenye kuhudumia shughuli za maendeleo. Lengo la mjadiliano hayo ni kusailia kipamoja hatua za kuchukuliwa kukabiliana na mgogoro hatari uliotokana na kupanda kwa kasi kwa bei za chakula, na nishati, katika soko la kimataifa katika wiki za karibuni.

Shambulio dhidi ya kiongozi wa Afghanistan lashtumiwa na KM

KM Ban Ki-moon ameshtumu vikali shambulio liliotukia Ijumapili katika mji wa Kabul, Afghanistan, dhidi ya Raisi Hamid Karzai wakati alipokuwa akiangalia paredi ya ushindi. Shambulio hilo pia lilisababisha vifo vya wanabunge wawili, na kuwajeruhi wanabunge tisa wengine, kitendo ambacho KM alisema kinaharamisha kabisa maadili ya kiutu.

Hapa na Pale

Mkutano wa Saba wa Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili umeingia kwenye wiki ya pili ya majadailiano katika Makao Makuu, ambapo masuala yanayotiliwa mkazo zaidi ni yale yanayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa umma wa kimataifa.

Mapigano Mogadishu kuchochea uhamaji mpya wa dharura

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliwaambia waandishi habari kwamba mapigano yaliozuka wiki hii katika mji mkuu wa Mogadishu, Usomali yamechochea tena uhamaji mpya wa raia. Watu 7,000 wanakadiriwa kulikimbia vurugu hilo wiki hii na kufululizia kwenye vitongoji viliopo karibu na Mogadishu. Uhamaji huu umeithirisha matatizo katika juhudi za kuhudumia kihali umma ambao unakadiriwa kufikia milioni moja. Idadi hii hutegemea kufadhiliwa misaada ya kihali na wahisani wa kimataifa na hadhi yao ni ile inayojulikana kama wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) waliong\'olewa makwao na kukosa mastakimu ya kudumu.

Siku ya Malaria Duniani

Kwa mara ya kwanza katika historia jamii ya kimataifa imeamua kuiheshimu tarehe 25 Aprili kila mwaka kuwa ni Siku ya Malaria Duniani. UM na mashirika yake kadha wa kadha yameandaa tafrija na hafla aina kwa aina ili kukumbushana juhudi zinazotakikana kutekelezwa kwa ushirika miongoni mwa Mataifa Wanachama, ili kufanikiwa kudhibiti bora maradhi ya malaria kote duniani.