Skip to main content

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Mkutano wa Saba wa Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili umeingia kwenye wiki ya pili ya majadailiano katika Makao Makuu, ambapo masuala yanayotiliwa mkazo zaidi ni yale yanayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa umma wa kimataifa.

Vile vile kikao cha pili cha Kamati ya Matayarisho ya Mkutano wa Mapitio wa Durban, kinaendelea mjini Geneva kwa mashauriano miongoni mwa wajumbe husika.

Kamati ya Matayarisho kwa Mkutano wa Mapitio ya Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Kudhibiti Silaha za Kinyuklia inaendelea pia na mijadala yake mjini Geneva, kuzungumzia taratibu bora za kuzuia uenezaji wa silaha za maangamizi ya halaiki katika dunia.

Vile vile Kamati dhidi ya Mateso inashauriana Geneva kwenye kikao chake cha 40, kuhusu hatua za kufuatiliwa kimataifa ili kufyeka kikamilifu matatizo ya mateso duniani.