Operesheni inayoungwa mkono na UM itawakinga watoto milioni 2 Zambia dhidi ya shurua
Kuanzia tarehe 09 hadi 14 Julai mashirika ya UM juu ya maendelo ya watoto UNICEF na afya WHO yatajumuika kuhudumia kipamoja chanjo dhidi ya shurua kwa watoto milioni 2 nchini Zambia.
Vile vile operesheni hii inatazamiwa kuwahudumia watoto lishe ya vitamini ili kuimarisha miili na pia kuwapatia vidonge vya kujikinga na ugonjwa wa minyoo.