Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serekali za eneo na UM zakubaliana 'ramani' ya kupambana na tatizo la njaa Pembe ya Afrika

Serekali za eneo na UM zakubaliana 'ramani' ya kupambana na tatizo la njaa Pembe ya Afrika

Wajumbe wa Serekali za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya Usomali na Uganda pamoja na wawakilishi wa UM walikutana kwa mazungumzo ya siku mbili mjini Nairobi (Kenya) wiki hii na walikubaliana kukabili kipamoja vyanzo vyenye kuchochea matatizo ya njaa katika maeneo ya Pembe ya Afrika.

Inaashariwa na wataalamu wa kimataifa kwamba bila ya kuidhibiti hali hii kwa ushirikiano kati ya mataifa ya eneo kuna hatari ya watu milioni 20 kuathiriwa vibaya kimaisha pindi patazuka tena maafa mengine makubwa katika siku za usoni.