Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Begi la sola lililotengenezwa kwa kutumia taka mali. Kipande cha sola kimeunganishwa na waya inayopokea nishati ya jua na kuingiza katika taa maalumu ambayo usiku hutumika kwa ajili ya kujisomea
UN News

Soma Bag: Mabegi ya mgongoni yanayotumia sola mkombozi kwa wanafunzi

Lengo namba nne la Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs linazungumzia juu ya elimu bora, yenye usawa na kutoa fursa kwa wote, na hicho ndicho kinachofanyika jijini Mwanza kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wamebuni mradi wa mabegi yanayokusanya nishati ya jua ili kuwasaidia wanafunzi waishio vijijini kujisomea nyakati za usiku.

WFP na serikali ya Madagascar zaungana mikono kubadilisha jamii za vijijini kusini mwa Madagascar.
© WFP Madagascar

Mradi wa RRT wa paneli za sola waangaza nuru Kusini mwa Madagascar:WFP

Kupitia mradi wa mabadiliko ya haraka vijijini (RRT) shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wake wameanzisha kituo maalum cha paneli za sola ambacho ni chanzo kikuu na endelevu cha maji na teknolojia ya mawasiliano ICT katika maeneo ya vijijini nchini Madagascar, hatua inayoruhusu upatikanaji wa huduma muhimu kama vile nishati, maji na mitandao ya kijamii kwa wakazi wa jamii hizo na kwa njia inayojali mazingira.

Sauti
2'35"
Wafanyakazi wa IOM wanaosimamia kambi wanafanya kazi katika baadhi ya kambi kubwa za watu waliokimbia makazi yao nchini Somalia.
IOM/Claudia Rosel

Mashirika ya UN yanavyohaha kuwasaidia waathirika wa mizozo na ukame Baidoa Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inasema idadi ya milipuko ya magonjwa iliyoripotiwa na dharura za kiafya zinazohusiana na tabianchi katika Ukanda wa Pembe ya Afrika zimefikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea karne hii, na hivyo kuzidisha janga la kiafya katika eneo ambalo watu milioni 47 tayari wanakabiliwa na njaa kali. 

Sauti
4'27"
WHO ukanda wa Ulaya ilisaidia mamlaka ya Kyrgyzstan kuweka taratibu zinazofaa za kupambana na COVID-19 katika vivuko vya mpakani
WHO-Europe

WHO ukanda wa ulaya waendesha kampeni ya utoaji chanjo ya homa ya mafua makali

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya ulaya tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali katikati ya mwezi Novemba mwaka 2022 wamebaini kuongezeka kwa wagonjwa wanaolazwa kutokana na magonjwa ya homa ya mafua makali au flu,  matatizo ya kupumua na COVID-19. Walio hatarini zaidi kupata maambukizi ya magonjwa hayo ni wahudumu wa afya pamoja na wazee, ndio maana wanaendesha kampeni ya kutoa chanjo.

Sauti
2'41"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kongamano la kiuchumi duniani WEF, mjini Davos, Uswisi.
© World Economic Forum

Hatuwezi kutatua zahma zinazotukabili katika dunia iliyogawanyika bila mshikamano: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.  

Sauti
2'45"
Mabalozi wema wa IFAD, Idris Elba (kushoto) na mkewe Sabrina Dhwore-Elba wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa IFAD Alvaro Lario baada ya kupokea tuzo ya mwaka 2023 ya  Crystal huko Davos, Uswisi kunakofanyika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani, WEF.
IFAD

Uwekezaji vijijini ndio mkombozi wa wakulima wadogo- Idris/Sabrina

Mabalozi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya kilimo duniani, IFAD, Sabrina Dhowre Elba na mumewe Idris Elba wamepatiwa tuzo ya mwaka 2023 ya Crystal au Crystal Award kutokana na uongozi wao wa kupaza sauti kwa niaba ya mamilioni ya wakulima wadogo maskini duniani kote ambao hufanya kazi kila siku kuzalisha theluthi moja ya chakula chote duniani.

Audio Duration
2'2"