Bilan, chombo cha habari kilichowezesha wanawake kushika hatamu ya habari Somalia
Hii leo tunakukutanisha na wanawake waandishi wa habari nchini Somalia wanaoendesha chombo chao kiitwacho Bilan. Chombo hiki kilianzishwa mwezi Aprili mwaka 2022 ili kuwapatia wanawake waandishi wa habari nguvu thabiti na ya ukweli pamoja na fursa ya kusongesha habari mpya na sauti mpya kwa hadhira nchini mwao Somalia.