Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mama wa jamii ya rendile akiwa na watoto wake Marsabit Kaskazini Mashariki mwa Kenya, baada ya kupokea msaada wa chakula (Marsabit)
Khoboso HarguraAdichareh/KPL

Ukame waongeza zahma ya kutokuwa na uhakika wa chakula Pembe ya Afrika:FAO

Ukame wa muda mrefu ulioghubika eneo la Pembe ya Afrika ikiwemo nchini Kenya unachochea hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula limeonya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO na kuongeza kuwa sasa watu milioni 12 hadi milioni 14 katika eneo hilo wako katika hatari wakati huu mazao yao yakiendelea kukauka na mifugo kudhoofika.

Sauti
2'4"
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linawasaidia wakulima wanaoishi katika mazingira magumu katika viunga vya nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima mimea ya dungusikakati isiyo
UN Video

Syria: Dungusikakati ni mkombozi kwa wafugaji na mazingira - FAO 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linawasaidia wakulima wanaoishi katika mazingira magumu katika viunga vya nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima mimea ya dungusikakati isiyo na miba ili waweze kuwalisha mifugo wao hasa nyakati za ukame. Taarifa ya Anold Kayanda inafafanua zaidi.  

Sauti
2'27"
Redio za zamani zikioneshwa katika jumba la makumbusho la Chihuly, Seattle, USA.
Unsplash/Rod Flores

Redio Kwizera: Kutoka kuhudumia wakimbizi kutoka Rwanda hadi mikoa mitano Tanzania  

Redio Kwizera ya wilayani Ngara mkoani Kagera Tanzania, tangu mwaka 1995 ilipoanzishwa na huduma ya majesuit wa kikatoliki kwa wakimbizi (JRS) kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ikiwa ni hatua ya kutaka kuwasaidia wakimbizi kukutana na wapendwa wao waliopoteana nao wakati wa kukimbia vita ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, imeendelea kuwa msaada kwa wakimbizi na wenyeji.  

Mlipuko wa volkano na Tsunami ya Tonga umeweka wazi mazingira hatarishi ya visiwa vidogo na Mataifa yanayoendelea (SIDS).
© Konionia Mafileo

UNICEF na serikali ya Japan kuwanusuru walioathirika na Tsunami na volcano Tonga 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Japani wametangaza ushirikiano mpya wa kuchangia dola milioni 1.25 kuisaidia serikali ya Ufalme wa Tonga kuhakikisha kuwa takriban watu 19,250 wakiwemo watoto 10,000 walioathiriwa na mlipuko wa volcano na tsunami hivi karibuni wanapata maji safi ya kutosha ya kunywa, mazingira safi , pamoja na afya njema.