Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Hadi sasa kimbunga Batsirai kimekatili maisha ya yawatu 121 na kutawanya wengine 29,000 : OCHA 

Kimbunga cha kitropiki, Batsirahi kimeleta uharibifu mkubwa pwani ya mashariki mwa Madagascar.
© WFP/Nejmeddine Halfaoui
Kimbunga cha kitropiki, Batsirahi kimeleta uharibifu mkubwa pwani ya mashariki mwa Madagascar.

 Hadi sasa kimbunga Batsirai kimekatili maisha ya yawatu 121 na kutawanya wengine 29,000 : OCHA 

Msaada wa Kibinadamu

Hadi kufikia sasa watu 121 wameshapoteza maisha na wengine 29,000 wametawanywa kutokana na kuzuka kwa kimbunga Batsirai , kwa mujibu wa taarifa mpya zilizo[pokelewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA. 

Taarifa hizo ambazo zimetolewa leo na shirika la kitaifa la Madagascar la kudhibiti majanga BNGRC zinasema idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa sababu ya kuanza kupokelewa taarifa mpya kutoka katioka maeneo ya vijijini hususan katika wilaya ya Ikongo jimbo la Fitovinany ambako maporomoko ya ardhi yamekatili maisha ya watu 87. 

OCHA inasema juhudi za kufikisha misaada muhimu ya kibinadamu zinaongezwa huku serikali ikikarabati miundombinu ya msingi iliyoharibiwa na kimbunga hicho. 

Jamii na mamlaka ziko katika tahadhari wakati hali mpya ya kitropiki inapotokea katika Bahari ya Hindi na ambayo inaweza kukumba pwani ya Kaskazini-Mashariki mwa Madagascar kesho Jumanne, tarehe 15 Februari, kama dhoruba ya kitropiki.