Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa UN wa SDGs kupanua wigo wa uwekezaji hadi dola milioni 114 kuchochea utekelezaji 

Jua linachomoza kwenye njia ya SDGs kwenye lango la jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
UN News/ Anton Uspensky
Jua linachomoza kwenye njia ya SDGs kwenye lango la jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.

Mfuko wa UN wa SDGs kupanua wigo wa uwekezaji hadi dola milioni 114 kuchochea utekelezaji 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo mfuko wa pamoja wa Umoja wa Mataifa wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs umetangaza upanuzi wa kihistoria wa uwekezaji wake kwa masoko matano mapya kote ulimwenguni na kwa kuongeza dola za Kimarekani milioni 54.5 katika uwekezaji wa ziada ili kuokoa malengo hayo ya maendeleo endelevu. 

Masoko hayo yamechaguliwa kutoka kundi la kimataifa la mawasilisho kutoka zaidi ya nchi 100, ambapo mapendekezo yaliyowasilishwa na Kenya, Madagaska, Macedonia Kaskazini, Suriname na Zimbabwe yaliibuka kuwa yenye nguvu zaidi, yenye athari zaidi, na yako tayari kwa uwekezaji kwenda kwenye jamii.  

Uwekezaji huu unajumuisha hatua muhimu na za pamoja za UN dhidi ya changamoto za kizazi hiki kuanzia , masuala ya afya katika ulimwengu ambao bado unakumbwa na janga la coronavirus">COVID-19 , uwezeshaji wa vijana hadi mabadiliko ya tabianchi.  

Usimamizi wa mchakato 

Chini ya uongozi wa waratibu wakaazi wa Umoja wa Mataifa, utekelezaji wa programu hizi utachochea azma ya Umoja wa Mataifa katika mataifa matano, na kuzindua kizazi kipya cha hatua shirikishi katika Umoja wa Mataifa, Serikali, mashirika ya kiraia na wawekezaji wa sekta binafsi. 

Akizungumzia uwekezaji huo Hiro Mizuno, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya fedha, ubunifu na uwekezaji endelevu, amesema, “Fedha hizo ziko zina fursa ya kuziba pengo katika kutoa na kuleta tija ya uwekezaji. Zinatoa mfano wa uwekezaji endelevu kwa kutumia nguvu ya masoko ili kuharakisha biashara, kuwezesha jamii, na kuwasafishia niia ya kujitosheleza.” 

Mwaka mmoja baada ya uzinduzi wa kwanza 

Tangazo hili linakuja chini ya mwaka mmoja baada tangu mfuko huo wa SDG kuzindua uwekezaji wake wa kwanza wa dola milioni 41 katika programu nne za kuleta mageuzi ya SDGs huko Fiji, Indonesia, Malawi, na Uruguay.  

Mwaka 2021, mpango wa dola milioni 17.9 nchini Papua New Guinea uliongezwa, na kwa kuongezwa kwa programu hizi mpya tano mpya, sasa jalada la uwekezaji wa kuchagiza malengo hayo la mfuko wa pamoja wa SDG utakua omeongezeka hadi hadi kufikia dola milioni 114.  

Kwingineko mfuko huo unatarajiwa kuongeza dola bilioni 5 za Kimarekani kusongeza uwekezaji wa SDGs katika program kwenye nchi 10. 

Utekelezaji wa uwekezaji huo 

Uwekezaji huo unajumuisha kuwepo kwa jukwaa linalohimiza hulka nzuri za masuala ya afya ya uzazi uzazi, na kuzuia VVU nchini Kenya kupitia utoaji wa dhamana ya miradi ya maendeleo.  

Dhamana hizo zitazalisha rasilimali ili kutoa msaada wa kifedha wa muda mrefu kwa wasichana kupata huduma ya afya ya ngono na uzazi.  

Nchini Madagascar itatumia zana mbalimbali za kifedha, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa hazina huru ya kufadhili miradi ya nishati mbadala na kupanua wigo wa ufikiaji wa watu kwa nishati nafuu na endelevu. 

Kwa ushirikiano na benki za maendeleo na taasisi za kifedha za ndani, Kituo kipya cha ufadhili cha kinachojali mazingifra cha Macedonia Kaskazini kilichoundwa kitatoa suluhu ya ufadhili ili kuharakisha mchakato wa kugeukia nishati mbadala na bora kwa kaya na biashara ambazo hazijahudumiwa.  

Suriname itatekeleza suluhu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha kibunifu cha udhamini cha kurahisisha upatikanaji wa mikopo, uanzishaji wa  biashara, na ushirika unaomilikiwa na wakulima ili kuendeleza mnyororo wa thamani endelevu na wenye mnepo kwa sekta ya mananasi nchini humo.  

Zimbabwe inatazamiwa kuzindua, mpango kabambe wa pamoja wa sekta ya umma na binafsi unaolenga kuwezesha ushiriki wa wanawake na vijana, hazina ya nishati mbadala ili kuanzisha maendeleo ya mfumo/miundombinu ya nishati mbadala nchini humo. 

Pia mfuko wa pamoja wa SDG umejitolea kufanya kazi na washirika mbalimbali na wafadhili ili kukusanya rasilimali zaidi kuweza kufadhili mapendekezo yaliyopitishwa ambayo yaliwasilishwa na Barbados, Ghana na Rwanda. 

 

TAGS:SDGs, Uwekezaji, UN. Malemgo ya maendeleo endelevu