Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Ndoa za utotoni zinazababisha wasichana kuacha shule
Photo: IRIN/Mujahid Safodien

Ukimuelimisha msichana umeielimisha Malawi: Chifu Kachindamoto

Nchini Malawi karibu nusu ya wasicha wote huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18 na hivyo hukosa elimu, hukabiliwa na ndoa za utotoni na pia athari nyingine kubwa za kiafya ikiwemo fistula na hata kupoteza maisha kutokana na kujifungua wakiwa na umri mdogo.  Sasa wanaharakati wamelivalia njuga sula hilo ambalo mzizi wake ni mila na desturi. 

Sauti
2'12"
Matumizi ya tumbaku ndio chanzo kinachozuilika cha saratani duniani
WHO

Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako- WHO

Kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa duniani ya kutovuta tumbaku keshokutwa Ijumaa, shirika la afya ulimwenguni, WHO  linaangazia madhara ya matumizi ya tumbaku kwa mapafu ya binadamu ikielezwa kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo vihusianavyo na utumiaji wa tumbaku vilihusiana na magonjwa kama saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa na Kifua Kikuu.

Sauti
2'30"