Skip to main content

Magonjwa yatokanyo na matumizi ya tumbaku yanagharimu dunia dola trilioni 1.4- WHO

Watu wengi waomeonywa kuhusu matumizi ya tumbaku.
WHO/ Regional Office for the Western Pacific
Watu wengi waomeonywa kuhusu matumizi ya tumbaku.

Magonjwa yatokanyo na matumizi ya tumbaku yanagharimu dunia dola trilioni 1.4- WHO

Afya

Gharama za magonjwa yatokanayo na matumizi ya tumbaku kila mwaka ni dola trilioni 1.4 kote ulimwenguni kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa leo Mei 31 kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku.

WHO imesema gharama hii ni kubwa lakini faida za kuacha uvutaji wa tumbaku kwa asilimia 20 ya watu duniani kote ambao wanatumia bidhaa hii ni kubwa zaidi, huku mapafu ya mvutaji tumbaku yakirekebika katika muda wa wiki mbili tu.

Shirika hilo limeongeza kuwa safari ni ndefu katika kutokomeza matumizi ya tumbaku kwani kufikia sasa ni asilimia 20 tu ya nchi ndizo zimefikia malengo ya kupunguza matumizi ya tumbaku. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi Dkt. Kerstin Schotte afisa wa kiufundi kitengo cha kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, NCDs amesema kuna hatua ambazo nchi zinaweza kuchukua ili kupunguza matumizi ya tumbaku ikiwemo

Sauti ya Dkt. Kerstin

“Kutokomeza aina zote za matangazo ya tumbaku na kampeni, kutoa tarifa kwa umma kuhusu hatari za kuvuta tumbaku, sote tunajua kwamba uvutaji wa tumbaku ni hatari lakini cha kushangaza utafiti wa kukabiliana na matumizi ya tumbaku unaonyesha kwamba watu wengi hawafahamu athari za tumbaku. Kuongeza bei ya bidhaa za tumbaku kutapunguza matumizi hususan miongoni mwa vijana kwanivijana hawataanza matumizi ya tumbaku iwapo hawataweza kugharamia na watumiaji wa tumbaku watapunguza matumizi ya bidhaa hizo.”

WHO imesema inategemea ushirikiano wa nchi wanachama kuweka mikakati hiyo kwa ajili ya kukabiliana na matumizi ya tumbaku.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako".

 

Wakati huo huo, Dkt. Isaac Maro ambaye ni tabibu, na mtafiti mshiriki na mkufunzi msaidizi katika chuo kikuu cha Tokyo nchini Japan katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amefafanua kwa kina madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku…

Sauti ya Dkt Isaac Maro

Sigara ni adhui nambari moja au chanzo kikubwa sana cha hitilafu kutokea kwenye chembe hai za mwili. Hitilafu ambayo inapekekea chembe hai za muili zigawanyike kwa kasi kuliko kawaida na zishindwe kufanya utaratibu wa kawaida wa kuzaliana na kufa. Kwa matokeo yake tunapata kitu kinachoitwa saratani. Kwa hiyo tunakuta sana kwa saratani nyingi sana  kwenye mwili wa mwanadamu zinatokana kwa kiwango kikubwa au zinatokea mara nyingi sana  kwa watu ambao wanatimia sigara kwa muda mrefu. Kwa hiyo hapa siotu saratani ya shingo lakini saratani ya kinywa inaweza kuonekana , tukishuka chini kwenye mapafu hiyo kwa ailimia mia moja saratani ya mapafu inatokana na matumizi ya muda mrefu ya sigara.

Kando mwa saratani, Dkt amesema  uvutaji sigara pia ni chanzo cha magonjwa mengine hatari kama

Sauti ya Dkt Isaac Maro

Unaweza ukapata maradhi ya moyo,lakini pia moyo kwasababu kazi yake ni kusafirisha damu, moyo pia inajipatia damu. Kuna changamoto ambayo inatokea kwenye mishipa ya damu, na mfumo wa damu ambayo inapelekea mabonge ya damu kutengenezawa. Sasa mabonge ya damu yanapotengenezwa  yanaweza kupekekea yakasukumwa halafu yakabanwa au yakaziba mrija ambao unapeka damu kwenye moyo wenyewe, kwahiyo  matokeo yake ni kwamba moyo utashindwa kufanya kazi, na matokeo yake ni kwamba  mtu ataumia unaweza ukapata kiharusi pia. Unaweka ukakutta kwamba hata ile mishipa kwenye ubongo nayo inaweza ikazibwa matokeo ni kwamba unapata kiharusi yaani stroke