Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukimuelimisha msichana umeielimisha Malawi: Chifu Kachindamoto

Ndoa za utotoni zinazababisha wasichana kuacha shule
Photo: IRIN/Mujahid Safodien
Ndoa za utotoni zinazababisha wasichana kuacha shule

Ukimuelimisha msichana umeielimisha Malawi: Chifu Kachindamoto

Haki za binadamu

Nchini Malawi karibu nusu ya wasicha wote huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18 na hivyo hukosa elimu, hukabiliwa na ndoa za utotoni na pia athari nyingine kubwa za kiafya ikiwemo fistula na hata kupoteza maisha kutokana na kujifungua wakiwa na umri mdogo.  Sasa wanaharakati wamelivalia njuga sula hilo ambalo mzizi wake ni mila na desturi. 

Ni sauti ya mmoja wa wanaharakati wakubwa wa kupigania haki za wasichana Malawi Chifu Teresa Kachindamoto kwa mtoto wa misho kati ya watoto 12 aliyebahatika kwenda kusoma ng’ambo, dhamira yake imekua kuhakikisha kila msicha nchini humo anapata elimu na kutopitia ndoa za utotoni.

Duniani kote wasichana zaidi ya milioni 700 walio hai hii leo wameolewa kabla ya kutimiza miaka 18 na wengi kuwa mama wangali watoto

KACHINDAMOTO

Nilirejea nyumbani nikiwa bado na mashaka endapo niko tayari kubeba jukumu hili, na wakati nikipita mtaani katika kiwanjani nikaona wasichana wakiangalia mpira wa miguu, kulikuwa na moja hasa aliyenigusa alikuwa amebeba mtoto mgongoni, nikaenda kuongea naye na akaniambia mtoto ni wake nilishutaka sana pale  aliponitajia umri wake alikuwa na miaka 13”

Kampeni ya Chifu Kachindamoto imeanza kuzaa matunda kwani hadi sasa amefanikiwa kutengua ndoa 3,500 za utotoni hususan katika jimbo la Kati la Malawi na kuwasaidia wasichana hao kuhitimu shule mara nyingi akiwasaidia karo ya shule kwasababu anaamini

KACHINDAMOTO 

Tunaweza kutokomeza kabisa ndoa za utotoni , kwani wasichana wakielimishwa wanakuwa na mustakabali bora”

Kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake UN Women, serikali ya Malawi, asasi za kiraia na viongozi wa kijadi alichangia kupitishwa kwa mabadiliko ya katiba mwezi Februari mwaka jana na kurekebisha sharia ya ndoa ambayo sasa imeongeza umri wa wasichana kuolewa kutoka miaka 15 hadi 18. Lakini kwake bado haitoshi

 KACHINDAMOTO 

Ninapambana kupandisha umri wa kisheria wa kuolewa kuwa miaka 21 ili wasichana wamalize shule , wasomesha wasichana ni moja ya hatua muhimu za kuvunja mzunguko wa umasikini na kuzuia matatizo ya muda mrefu kwa wanawake”

Ingawa bado hilo halijatimia Chifu Kachindamoto anasema, alutakontinua mapambano bado yanaendelea Malawi hadi kila msichana asome, awe huru na ndoa za utotoni na aweze kujitegemea

TAGS:Malawi, wasichana, elimu, ndoa za utotoni chifu Theresa Kachindamoto