Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya ulinzi wa amani ni ya kila mtu la msingi ni kuwa tayari: Mrakibu Mlay

Akisaidiwa na wenzake wawili, Angela Ama Agyeman Sesime (katikati) wa Ghana, Polisi mshauri wa UNAMID akiandika ripoti baada ya doria katika kambi ya Zam Zam ya kuwahifadhi wakimbizi wa ndani eneo la Darfur Kaskazini, Sudan, Oktoba 2010.
UN/Olivier Chassot
Akisaidiwa na wenzake wawili, Angela Ama Agyeman Sesime (katikati) wa Ghana, Polisi mshauri wa UNAMID akiandika ripoti baada ya doria katika kambi ya Zam Zam ya kuwahifadhi wakimbizi wa ndani eneo la Darfur Kaskazini, Sudan, Oktoba 2010.

Kazi ya ulinzi wa amani ni ya kila mtu la msingi ni kuwa tayari: Mrakibu Mlay

Amani na Usalama

Ulinzi wa amani si chaguo ni wajibu ambao kila mtu katika jamii anapaswa kuuvaa, kwani bila amani jamii husambatarika. Nani katoa kauli hiyo tuungane na Jason Nyakundi  anatupasha zaidi

Kauli hiyo imetolewa na mrakibu mwandamizi wa polisi Martha Neema Mlay kutoka nchini Tanzania ambaye ni miongoni mwa walinda amani wanawake waliowahi kushiriki kwenye opresheni za Umoja wa Mataifa katika mpango wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni Darfur nchini Sudan ,UNAMID. Ameyasema hayo aplipozungumza kuhusu umuhimu wa amani na operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na wanafunzi mbalimbali wa sekondari jijini Dar es salaam.

Ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya ulinzi wa amani duniani siku iliyobeba kaulimbiu ya “kulinda raia na jamii zao”, Bi Mlay amesema, wanawake walinda amani wanamchango mkubwa katika operesheni hizo

SAUTI YA MRAKIBU MARTHA NEEMA MLAY

 

Kwahiyo kwenye shughuli za ulinzi wa Amani, kuna mambo mengi na  nafasi ya mwanamke kule ni kubwa. Na huiwakilishi tu nchi , lakini hata wewe mwenyewe  unajifunza tamaduni mbalimbali na unakutana na mataifa mbalimbali na unajuwa wale watu wanaishije.

Kwa hiyo nimekutana na watu wa Yemen , nimekutana na watu Jordan, nimekutana na watu wa Sierra Leone  na wengine wanatoka sijui Cameroun . kwa hiyo licha ya kwamba umeiwakilisha nchi , umeonyesha mchango wako kwenye Umoja wa Mataifa. Lakini wewe mwenyewe unakuwa umepanua uwezo wako wakuelewa, kwasababu umekutana na watu wa mataifa tofautitofauti. Umefanya kazi tofauti na mlivyozoea kufanya  kwenye nchi yako.

Kwahiyo ukirudi nchini kwako unakuwa  na mchango chanya  kwenye nchi yako kutokana na kile ulichojifunza kule ulikotoka. Kwa hiyo wito wangu kwenu ni tulinde amani ya Tanzania na tusikubali kuipoteza. Na tujuwe kwamba ulinzi wa amani upo, ni  kazi  ya kila mmoja  na nafasi zipo. Kwa hiyo tujifunze, tusome kwa bidii wakati utakapofika tushiriki, tusiogope.

 

Nao wanafunzi walioelimishwa kuhusu umuhimu wa amani wana maoni gani?

Naitwa Zofai Idrisa  Niko kidato cha tano naangalia sehemu ambazo hazina amani zina vita, watu hawaishi vizuri, inakwamisha  vitu vingi sana, maendeleo kwanza, watoto wanakuwa hawaendi shule kwa hiyo amani ni muhimu sana.

Naitwa  Grayson Robert mwanafunzi kidato cha tano EGM, ukizingatia kauli mbiu mwaka huu ambayo inasema kulinda amani kulinda na wanainchi wake. Ni njia nzuri sana kwani inafikisha ujumbe moja kwa moja kwa wananchi kudumisha amani na kuwalinda watu wake. Kwasababu tunaangalia hasa hasa dunia ya sasa hivi jinsi gani mashariki ya mbali huko kunapotokea vita na madhara yake. Kwa hiyo sisi kama wananchi na UN kama UN hii inatusaidia sana kudumisha amani ya nchi na amani ya dunia kwa ujumla.