Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaid ya dola bilioni 3 zahitajika msumbiji kwa ujenzi mpya baada ya vimbunga Idai na Keneth:UNDP

Mwanamke akiwa amebeba mwanaye akitembea kwenye makazi ya watu waliotawanywa na vimbunga Idai na Kenneth kwenye jimbo la Beira nchini Msumbiji (28 Mei 2019)
UNICEF/Karel Prinsloo
Mwanamke akiwa amebeba mwanaye akitembea kwenye makazi ya watu waliotawanywa na vimbunga Idai na Kenneth kwenye jimbo la Beira nchini Msumbiji (28 Mei 2019)

Zaid ya dola bilioni 3 zahitajika msumbiji kwa ujenzi mpya baada ya vimbunga Idai na Keneth:UNDP

Tabianchi na mazingira

Serikali ya Msumbiji leo inafanya mkutano wa kimataifa wa ufadhili mjini Beira kwa ajili ya kuomba msaada wa  ujenzi mpya wa kijamii, uzalishaji na miundombinu baada ya athari za vimbunga Idai na Keneth.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linalosaidia kuendesha mkutano huo Msumbiji inahitaji dola bilioni 3.2 zitakazotumika katika ujenzi mpya kwenye majimbo yaliyoathirika zaidi na vimbunga ya Sofala, Manica, Tete, Zamezia, Inhambane, Nampula na cabo Delgado ambako jumla ya watu milioni 1.85 waliathirika na vimbunga hivyo.

Mkutano huo wa siku mbili utakaomalizika keshoi Juni Mosi umeandaliwa na kamati ya ujenzi mpya ilianzishwa na serikali baada ya vimbunga Idai na Keneth kwa lengo la kusaidia ujenzi mpya na kuzijengea mnepo jamii zilizoathirika vibaya na vimbunga hivyo ambavyo kwa pamoja vimekatili maisha ya watu 600 na kuwaacha mamilioni wakihitaji msaada wa kibinadamu.

Akizungumzia umuhimu wa mkutano huo na ukusanyaji fecha za ufadhili mkuu msaidizi na mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa UNDP Ahunna Aziakonwa amesema“Binafsi nimeshuhudia athari za kimbunga Idai nilipozuru hivi karibuni maeneo yaloiyoathirika Msumbiji. UNDP inaunga mkono juhudi za serikali ya Msumbiji za kufanikisha ujenzi mpya endelevu na kuzijengea jamii mnepo dhidi ya majanga”

Shule ambayo sasa watoto wengi wanahudhuria kwenye Wilaya ya Namacurra jimbo la Zambezia nchini Msumbiji baada ya shule nyingi kuharibiwa na vimbunga
@UH-HABITAT
Shule ambayo sasa watoto wengi wanahudhuria kwenye Wilaya ya Namacurra jimbo la Zambezia nchini Msumbiji baada ya shule nyingi kuharibiwa na vimbunga

Msingi wa mkutano huo wa ufadhili ni tathimini ya mahitaji ya baada ya majanga hayo (PDNA) iliyoendeshwa na UNDP, Muungano wa Ulaya, Benko ya dunia  na Benki ya Maendeleo barani afrika (ADB). Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Msumbiji Anna Comoana “Leo siku ya kwanza ya mkutano inajikita na majadiliano ya masuala ya kiufundi na kesho Juni Mosi ndio utajikita na ahadi za msaada kwa mujibu wa vipaumbele vilivyoainishwa na Rais Felipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji.”

UNDP inasaidia mkutano huo hasa katika upande wa será na masuala ya kiufundi , na katika ujenzi mpya itashirikiana kwa karibu na wadau wote na kusaidia kzijengea jamii za nchi hiyo mneno.

 Mkutano huo uliofunguliwa na Rais Felipe Nyusi umewaleta pamoja washiriki takriban 700 kutoka mashirika ya kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia.