Mahakama ya kuhamahama yapeleka haki Malakal, Sudan Kusini.
Kwa zaidi ya kipindi cha siku tatu, mahakama ya kuhamahama inayofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imekuwa katika mji wa Malakal jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ili kushughulikia kesi kadhaa zikiwahusisha watu ambao walitenda makossa makubwa yakiwemo kesi mbili za unyanyasaji wa kingono na moja ya unyanganyi kwa kutumia silaha.