M23 wanaendelea kutekeleza ukatili Kivu Kaskazini: Türk
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amehitimisha ziara yake rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mjini Kinshasa jana Alhamisi 18 Aprili.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amehitimisha ziara yake rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mjini Kinshasa jana Alhamisi 18 Aprili.
Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapigano.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hali ya usalama inazidi kudorora kila uchao kwenye jimbo la Kivu Kaskazini kufuatia kuibuka tena kwa mapigano makali kati ya waasi wa kundi la M23 na jeshi la serikali FARDC.
Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.
Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.
Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali.
Ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuhusu haki za binadamu, (UNJHRO) imeripoti ongezeko la asilimia 2 la vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo kwa mwezi wa Februari mwaka huu ikilinganishwa na mwezi uliotanguliwa wa Januari.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika.