DRC: Oktoba pekee zaidi ya watu 300,000 wafurushwa Kivu Kaskazini
- Ghasia zafurusha watu 300,000 Kivu Kaskazini
- Jumla ya waliofurushwa Mashariki ya DRC zaidi ya milioni 6
- Watu 140,000 wakosa misaada ya kibinadamu
Japan imelipatia shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Tanzania msaada wad ola za kimarekani 500,000 kwa ajili ya huduma za usafi na kujisafi, WASH, halikadhalika makazi salama, maji na mahitaji mengine muhimu kwa wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), walioingia mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) unasikitishwa na mapigano kati ya wanamgambo wa M23, wanajeshi wa Congo na miungano ya makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakitokea kila siku tangu mwanzoni mwa Oktoba katika jimbo la Kivu Kaskazini, ameeleza Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Machafuko yanayoshika kasi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, yameendelea kukatili Maisha ya watu , kujeruhi na kuwalazimisha wengi kufungasha virago na kuzikimbia nyumba zao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake.
Hivi sasa dalili za mzozano wa moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda zi wazi kutokana na pande hizo kuendelea kulaumiana juu ya uungaji mkono wa makundi yaliyojihami Mashariki mwa DRC, wakati huu ambapo hali ya amani inazidi kuzorota.
Likijibu ombi lililotolewa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, la kutaka kuharakishwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, kuondoka kuanzia mwisho wa 2023, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limetangaza kuwa liko "tayari kuamua, ifikapo mwisho wa 2023, juu ya mustakabali wa MONUSCO, uondoaji wake wa kimaendeleo, uwajibikaji na uendelevu na hatua madhubuti na za kweli zinazopaswa kuchukuliwa kama kipaumbele kutekeleza uondokaji huo”.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umewasimamisha kazi baadhi ya walinda amani wake kufuatia ripoti za ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kazi.
Visa vya kutisha vya ukatili dhidi ya watoto hususan waliofurushwa makwao maeneo mbalimbali duniani vimesababisha viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa kurejelea wito wao wa ulinzi wa watoto na kuhakikisha wakati wowote ule haki zao zinalindwa kwa mujib uwa sheria ya kimataifa, na wakati huo huo watendao uhalifu huo wasikwepe sheria.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) unashiriki katika maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo tayari umeshasaidia usafirishaji wa nyaraka za uchaguzi, halikadhalika mafunzo kwa polisi wa kitaifa ili uchaguzi huo uwe huru na ufanyike kwa amani.