Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Baadhi ya uharibifu wa mazingira na mali uliofanywa na mafuriko huko Kalehe, jimboni Kivu Kusini, DRC mwezi Mei, 2023.
UN News/George Musubao

Baada ya mafuriko Kalehe, DRC, wananchi wahamasishwa kuyalinda mazingira

Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu.

 

Sauti
4'38"
Wadau wa lugha ya Kiswahili wakizungumza na Flora Nducha hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani.
UN News

Lengo letu ni kuhakikisha kila mtu Afrika anakijua na kukizungumza Kiswahili-Wadau

Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yamewadia ni wiki ijayo tarehe 7 ya mwezi Julai ambapo wadau wote wa kiswahili duniani kuanzia kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, kwenye Mataifa wazungumzaji wa lugha hii adhimu hadi ughaibuni mambo yatakuwa bambam, lakini hapa kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa maandalizi yamefikia wapi? Na nini kitajiri? Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imewaalika wadau wa Kiswahili hapa kwenye makao makuu kufahamu maandalizi yanaendeleaje.

Watoto wakiteka maji katika kambi ya wakimbizi wa ndani, Rusayo, DRC.
George Musubao

Siku ya Wakimbizi Duniani, wakimbizi wa ndani DRC wanasemaje?

Hapa ni kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rusayo iliyoko takribani kilometa 17 magharibi mwa mji wa Goma, jimboni Kivu kaskazini, Mashariki mwa DRC, ndivyo anavyoanza kusimulia George Musubao, Mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC aliyesafiri kutoka Beni hadi kambini Rusayo kuzungumza na wananchi ambao wamelazimika kukimbia makazi yao na sasa maisha yao yanategemea hisani za jumuiya ya kimataifa kupitia Umoja wa Mataifa. 

Ujumbe wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) watembelea vikosi vya FIB MONUSCO nchini DRC.
Abubakar Muna/JWTZ

Ujumbe wa jeshi la wananchi la Tanzania watembelea vikosi vya FIB nchini DRC

Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Brigedia Jenerali Geoge Mwita Itang’are akiwa ameambatana na ujumbe wake kutoka makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania (JWTZ) kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Tanzania Jenerali John Jacob Mkunda umefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya majeshi ya Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  DRC ujulikanao kama MONUSCO kwenye eneo la Goma na kukutana na kamanda wa vikosi hivyo Luteni Jenerali Otavio Rodrigues De Miranda Filho.

Prime Metal, mnufaika wa mradi wa RAPID IMPACT PROJECT nchini DRC ambaye aliwahi kutekwa nyara na kuokolewa juhudi za MONUSCO .
Byobe Malenga/UN News

Nilitekwa nyara na waasi, lakini MONUSCO ilinikomboa- Mwananchi DRC 

Wiki hii dunia imeadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Tangu mwaka huo zaidi ya wafanyakazi milioni mbili waliovalia sare kijeshi na raia wamesaidia nchi kuhama kutoka vita hadi kwenye amani. Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umekuweko tangu mwaka 2000, ikimaanisha mwaka huu ni miaka 23.