Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya M23 na makundi mengine kikwazo kwa misaada ya kibidamu DRC

Watoto wakicheza katika kambi ya Awar huko Mahagi, jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
IOM
Watoto wakicheza katika kambi ya Awar huko Mahagi, jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mapigano ya M23 na makundi mengine kikwazo kwa misaada ya kibidamu DRC

Amani na Usalama

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) unasikitishwa na mapigano kati ya wanamgambo wa M23, wanajeshi wa Congo na miungano ya makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakitokea kila siku tangu mwanzoni mwa Oktoba katika jimbo la Kivu Kaskazini, ameeleza Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Bwana Stéphane Dujarric, akizungumza na waandishi wa habari mjini New York leo (30 Oktoba), amesema, "Mapigano haya yanayotokea katika maeneo ya Masisi, Rutshuru, na Nyiragongo, yanawakilisha ongezeko kubwa la vita mashariki mwa Congo. Pia ni tishio kubwa kwa oparesheni za kutoa misaada ya kibinadamu na kwa maeneo yanayohifadhi watu waliofurushwa kwenye makazi yao pembezoni mwa Goma.” 

Pia Dujarric amesema, "Walinda amani walituma Kikosi cha Majibu ya Haraka huko Rutshuru kulinda raia. Kwa kufanya kazi kwa karibu na wanajeshi wa DRC na Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kufanya doria kulinda Goma. Pia wameanzisha maeneo ya usalama kuzunguka vituo vya usambazaji wa misaada ya kibinadamu karibu na kituo chetu cha Kitchanga na kusindikiza utoaji wa bidhaa zisizo za chakula na usaidizi mwingine wa kibinadamu katika eneo hilo, ambapo takriban wakimbizi wa ndani 25,000 wanatafuta ulinzi karibu na kituo cha MONUSCO.”