Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
UNICEF, Microsoft na Cambrigde watangaza Pasipoti ya kujifunza
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Microsoft hii leo mjini New York Marekani wametangaza upanuzi wa jukwaa la kimataifa la kujifunza kuwasaidia watoto na vijana ambao wameathiriwa na COVID-19 kuendelea na elimu yao wakiwa nyumbani.
Tutahakikisha wakimbizi wako salama dhidi ya COVID-19 :UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linafanya kila juhudi kuhakikisha linanusuru maisha ya mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Magharibi na Kati yaliyo hatarini kutokana na changamoto mpya iliyozuka ya virusi vya Corona au COVID-19.
Shirika hilo linasema nchi 21 za kanda hiyo ambazo nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita, wakimbizi na wakimbizi wa ndani zinahitaji msaada ili kukabiliana na janga jipya linaloitikisa dunia hivi sasa.
IFAD inastahili kushinkwa mkono ili kusaidia wakulima Idri na Sabrina Elba
Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD leo wamezindua ombi la dola milioni 200 ili kuzisaidia jamii za vijiji kukabiliana na mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19
20 APRILI 2020
Katika Jarida la Habari hii leo Flora ucha kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea
- Serikali ya Tanzania yaitikia wito wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO na leo imezindua mkakati wa ufundishaji kupitia teknolojia ya Radio na Televisheni kuhakikisha watoto wanasoma wakati huu wa COVID-19
- Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD Idris Elba na mkewe sabrina Elba leo wamezindua mfuko na ombi la dola milioni 200 kuwasaidia wakulima vijijini wakati huu wa janga la Corona ili kuhakikisha uhakika wa chakula
Mabalozi wema wa IFAD wazindua ombi la dola milioni 200 kuzisaidia jamii za vijijini dhidi ya COVID-19
Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD leo wamezindua ombi la dola milioni 200 ili kuzisaidia jamii za vijiji kukabiliana na mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19
UNHCR yaongeza juhudu kunusuru maisha ya mamilioni Afrika dhidi ya COVID-19
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linafanya kila juhudi kuhakikisha linanusuru maisha ya mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Magharibi na Kati yaliyo hatarini kutokana na changamoto mpya iliyozuka ya virusi vya Corona au COVID-19.
Kwa pamoja tutalishinda janga la COVID-19:Guterres
Tunakabiliana na tatizo lisilo na mithili yake. Ili kulishinda, ni sharti tuungane. Tatizo hili ni mliko wa janga la virusi vya corona au COVID-19
Tamasha la Dunia moja, pamoja nyumbani kufanyika leo:WHO
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHODkt. Tedros Ghebreyesus na mawanamuziki nyota duniani Lady Gaga Pamoja na Hugh Evans kutoka mradi wa raia wa kimataifa au Global Citizen Ijumaa wametangaza kwamba “ wanamuziki wengi mashuhuru duniani , wasanii wa vichekesho na wahudumu wa kibinadamu watashiriki katika tamasha maalum la kimataifa mtandaoni lijulikanalo kama “One Worl, Together at Home “ likimaanisha dunia moja, wote kwa pamoja majumbani litakalofanyika hii leo.
AU na Afrika wameonyesha umoja na uongozi ambao ni nadra hivi sasa kuhusu COVID-19:UN
Muungano wa Afrika AU na bara zima la Afrika wameonyesha umoja na uongozi vitu viwili ambavyo ni nadra sana latika nyakati hizi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo.
Tuko watu tisa katika chumba kimoja, tunaihofia COVID-19- Qusai Al-Khatib
Wakati janga la COVID-19 likiendelea kuuzingira ulimwengu, familia za raia wa Syria zilizoko hatarini zina hofu zaidi kwa sababu zinaendelea kuishi katika mazingira yenye msongamano mkubwa na kukiwa na nafasi finyu ya kupata huduma za afya.