Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

22 APRILI 2020

Leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa unasema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kengele ya kuiamsha dunia kuchukua hatua kulinda sayari hiyo na watu wake  hasa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya mama sayari dunia

- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na jiji la Nairobi wanachukua hatua kudhibiti kusambaa wa virusi vya corona au COVID-19, kwenye makazi dunia ya Kibera.

Sauti
12'44"
Wakimbizi wa Burundi katika  makazi ya Mulongwe huko Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
UNHCR/Georgina Goodwin

Watu 80,000 waathiriwa na mafuriko makubwa DRC

 Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Andrej Mahecic hii ameviambia vyombo vya habari mjini Geneva Uswisi kuwa UNHCR inashirikiana na mamlaka pamoja na wadau nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoa msaada kwa watu 80,000 ambao wameathiriwa na mafuriko makubwa katika jimbo la Kivu Kusini. 

21 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa , EU na USAID wamesema janga la virusi vya Corona au COVID-19 limeweka njiapanda mustakbali wa chakula duniani hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa haraka kuepusha baa la njaa

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatoa mafunzo likishirikiana na wadau kuhakikisha wakimbizi wanakingwa dhidi ya COVID-19

Sauti
11'24"