20 APRILI 2020

20 Aprili 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora ucha kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea

- Serikali ya Tanzania yaitikia wito wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO na leo imezindua mkakati wa ufundishaji kupitia teknolojia ya Radio na Televisheni kuhakikisha watoto wanasoma wakati huu wa COVID-19

- Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD Idris Elba na mkewe sabrina Elba leo wamezindua mfuko na ombi la dola milioni 200 kuwasaidia wakulima vijijini wakati huu wa janga la Corona ili kuhakikisha uhakika wa chakula

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeongeza juhudi zake Afrika Magharibi na Kati ili kunusuru maisha ya mamilioni ya watu waliotawanywa, wakimbizi na wakimbizi wa ndani dhidi ya COVID-19

-Makala yetu leo inatupeleka Tanga  Saa Zumo kutoka Redio washirika Pangani FM anazungumza na mkulima kuhusu changamoto za mabadiliko ya tabianchi

-Na mashinani tunabisha hodi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC utamsikia biti wa miaka 16 Docile Batumike  katika harakati za uelimishaji wa kupambana na janga la Corona.

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
13'24"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud