Tamasha la Dunia moja, pamoja nyumbani kufanyika leo:WHO

18 Aprili 2020

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHODkt. Tedros Ghebreyesus na mawanamuziki nyota duniani Lady Gaga Pamoja na Hugh Evans kutoka mradi wa raia wa kimataifa au Global Citizen Ijumaa wametangaza kwamba “ wanamuziki wengi mashuhuru duniani , wasanii wa vichekesho na wahudumu wa kibinadamu watashiriki katika tamasha maalum la kimataifa mtandaoni lijulikanalo kama “One Worl, Together at Home “ likimaanisha dunia moja, wote kwa pamoja majumbani litakalofanyika hii leo.

Dkt. Tedros amesema hii ni fursa maalum ya “kuleta furaha na matumaini kwa nyumba za watu wote kote duniani ambao Maisha yao yamepinduliwa juu chini na janga la virusi vya corona au COVID-19.”

Ameongeza kuwa ni “fursa ya kuonyesha mshikamano na wahudumu walio msitari wa mbele na kuchagiza wadau mbalimbali wakiwemo wahisani sekta binafsi,na serikali ili kusaidia mfuko wa hatua za mshikanao dhidi ya COVID-19, ambao unatiwa nguvu na wakfu wa Umoja wa Mataifa na mfuko wa uhisani wa Uswis.”

Hadi sasa mfuko huo wa mshikamano kwa ajili ya kupambana na COVIDI-19 umeshakusanya dola milioni 150 kutoka kwa watu Zaidi ya 245,000, mashirika na wakfu mbalimbali.

Kutoka kushoto Princess Dina Mirad wa Jordan, Mkuu wa WHO Dkt, Tedros Ghebreyesus, mwanaharakati wa afya ya akili na mama wa Lady Gaga Bi. Cynthia Germanotta na mwanamuziki wa Nigeria Korede Bello  wakati waliposhiriki walk the talk mjini Geneva Uswis.
Twitter
Kutoka kushoto Princess Dina Mirad wa Jordan, Mkuu wa WHO Dkt, Tedros Ghebreyesus, mwanaharakati wa afya ya akili na mama wa Lady Gaga Bi. Cynthia Germanotta na mwanamuziki wa Nigeria Korede Bello wakati waliposhiriki walk the talk mjini Geneva Uswis.

Lady Gagaga kwa upande wake amesema “Viongozi, wadau wengine wa mashirika binafsi, wasanii wa kila aina na watu wa kila taifa wamekusanya nguvu pamoja kuandika barua ya upendo kwa dunia n ani bariaua ya upendo kwa madakrati. Barua ya upendo kwa wauguzi wet una wahudumu wengine wa afya ambao wanahatarisha Maisha yao kwa ajili ya kunusuru ya kwetu, kwa madereva wanaosafirisha vifa muhimu, wafanyakazi wa maduka ya vyakula, wafanyakazi wa viwandani, wafanyakazi wa huduma za usafiri wa umma, wafanyakazi wa post ana wafayakazi wa migahawa na hoteli pia. Tunasherehekea ujasiri na ushujaa wenu.”

Naye Evans kutoka Global Citizen anasema “fedha zitakazokusanywa leo Jumamosi zitakwenda kusaidia mashirikaya hisani ya kijamii, kutoa vifaa vya kujikinga PPE kwa wahudumu wa afya duniani kote,kama  barakoa, vifaa vingine vya kujilinda, magauni ya hospitali, miwani ya kitabibu vitu ambavyo wahudumu wa afya wanastahili kuvipata. Wahudumu wetu wa afya wanastahili msaada wet una tunajua kwamba endapo kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake tutalishinda janga hili.”

Tamasha hilo la “One World Together at Home” linafanyika leo Jumamosi Aprili 18 na litajumuisha washiriki kama Elton John, Adam Lambert, Alicial Keys, Annie Lennox, Billie English na wengine wengi likiongozwa na Lady Gaga.

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter