Viongozi wa mashirika ya UN waungana na wadau kupigania mabadiliko ya elimu
Viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia watoto, UNICEF, la kupambana na UKIMWI, UNAIDS na la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kwa kushirikiana na wadau wametoa mawazo yao kuhusu kubadilisha mfumo wa elimu ili uendani na wakati na pia usimwache yeyote nyuma bila kujali aliko na hali yake.