Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya RapidPro iliyoletwa na UNICEF imeokoa watoto wetu Turkana nchini Kenya – Wazazi

Huduma ya RapidPro iliyoletwa na UNICEF imeokoa watoto wetu Turkana nchini Kenya – Wazazi

Pakua

Kaunti ya Turkana nchini Kenya inakabiliwa na ukame wa muda mrefu. Ili kusaidia kuimarisha mifumo ya lishe, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, nchini Kenya limeanzisha mfumo wa simu za mkononi uitwao RapidPro. Huduma hii huwezesha vituo vya afya kushirikishana ujumbe wa lishe na wafanyakazi wa kujitolea wa afya ya jamii, ambao huripoti taarifa na takwimu mbalimbali za kiafya kuhusu jamii zao. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Anold Kayanda
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
© UNICEF/Yves Nijimbere