Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya ulinzi kutoka Bunge la Tanzania yazuru shughuli za MINUSMA

Kamati ya ulinzi kutoka Bunge la Tanzania yazuru shughuli za MINUSMA

Pakua

Kamati ya kudumu ya ulinzi na usalama ya Bunge la Tanzania imefanya ziara nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ili kujionea shughuli za ulinzi wa amani zinazotekelezwa na vikosi vya nchi mbalimbali kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazochangia ulinzi wa amani kwa kupeleka wanajeshi walinda amnai ambapo kwa sasa kikosi kinachohudumu nchini CAR ni kikosi cha 5 kutoka tangu Tanzania ilipanza kupeleka walinda amani nchini humo ili kusaidia kulinda raia na kusimamia amani. Meja Asia Hussein ni Afisa Habari wa kikosi hicho anaripoti kuhusu ziara hiyo akiwa katika mji mkuu wa CAR, Bangui.  

Audio Credit
Anold Kayanda/Asia Hussein
Audio Duration
3'30"
Photo Credit
Photo: MINUSCA/Honorine Guehi Niare Yao