Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mienendo ya ujanani inavyoweza kuwa baraka au balaa uzeeni -Sehemu ya kwanza

Mienendo ya ujanani inavyoweza kuwa baraka au balaa uzeeni -Sehemu ya kwanza

Pakua

Mienendo ya mtu katika ujana wake hutoa matunda yake au machungu wakati wa uzee, anasema mzee mmoja nchini Uganda aitwaye Peter Semiga ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 80. 

Mienendo hiyo ambayo kulingana na uzoefu wake ni hatari kwa mustakbali wa kijana ni pamoja na tabia mbaya ya matumizi ya pesa, uvutaji wa sigara, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo vingine. 

Ili kufahamu kwa undani mawaidha ya kuepuka kero uzeeni baada ya kula vyote katika kipindi kifupi cha ujana, ungana na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego kwa sehemu ya kwanza ya makala akimhoji Mzee Peter Semiga. 

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
UN News/ John Kibego