Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/ John Kibego

Wasichana wapata stadi za kuwasaidia kustawi licha ya  COVID-19 na mafuriko nchini Uganda

Mafuriko yanayozidi kukosesha watu wengi makazi hasa katika maeneo ya ziwa Albert nchini Uganda sambamba na athari za COVID-19 yameathiri ustawi wa watu katika matabaka mbalimbali.Vijana hasa wa kike wanaripotiwa kuingia katika hatari za kubakwa, na kutumbukia kwenye ndoa za utotoni na madhara yake. Kikundi cha Kaiso Women’s Group kwenye Ziwa Alebrt wilayani Hoima wanajitahidi kupambana na hali hiyo kwa kuwsafunza baadhi ya wasichana pamoja na wanawake ufundi cherehani na utengenezaji wa sabuni miongoni mwa mengine ambayo tayari vimeleta nuru.

Sauti
3'38"