COVID-19 isitufanye tukayasahau mazingira-Clara Makenya

22 Juni 2020

Tangu mlipuko wa virusi vya corona ulipoanza kusambaa duniani kote, vipaumbele vya nchi nyingi vimebadilika. Ungana na Hilda Phoya wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania ili kufahamu uhusiano hasi na chanya wa COVID-19 kwa mazingira katika makala hii ambayo Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Tanzania, anaeleza wasiwasi wake kuwa huenda kutokana na nchi mbalimbali kuelekeza nguvu zake katika mapambano na COVID-19 kuna uwezekano wa mazingira kusahaulika katika nyakati hizo ambazo mabadiliko ya tabianchi ni janga lingine kubwa linalopaswa kuendelea kupewa kipaumbele. 

 

Makala hii imetayarishwa na UNIC Dar.

Audio Credit:
UNIC Dar es Salaam/Hilda Phoya
Audio Duration:
3'54"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud