Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 imeongeza ugumu katika changamoto za awali za watu wenye ualbino lakini na mwanga upo

COVID-19 imeongeza ugumu katika changamoto za awali za watu wenye ualbino lakini na mwanga upo

Pakua

Katika kipindi cha takribani miaka kumi nyuma kufikia mwaka 2015 nchini Tanzania kulisheheni matukio mengi ya kutisha yaliyohusisha mauaji au kujeruhiwa kwa kukatwa viungo watu wenye ualbino kutokana na imani za kishirikina. Wadau wa masuala ya haki za watu wenye ualbino wanasema kama si mlipuko wa COVID-19 kuwaongezea matatizo katika changamoto za muda wote kama vile uoni hafifu na matatizo ya ngozi, watu wenye ualbino walikuwa wameanza kuuona unafuu wa maisha kutokana na kupungua kwa matukio ya mauaji dhidi yao. Kuhusu hayo na mengine mengi, Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam amekutana na mdau wa haki za watu wenye ualbino ili kuangazia  baadhi ya changamoto za COVID-19 kwa watu wenye ualbino, pamoja na hatua zilizofikiwa kupambana na mauaji ya watu hao.

Audio Credit
Loise Wairimu/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
4'12"
Photo Credit
UN News/Video capture