Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumejisikia fahari kutokana na hatua ya kuhamasisha kazi yetu itambulike kama kazi ya muhimu-Mabaharia 

Tumejisikia fahari kutokana na hatua ya kuhamasisha kazi yetu itambulike kama kazi ya muhimu-Mabaharia 

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kuhusu siku ya baharia inayoadhimishwa hii leo kama ilivyo ada ya kila tarehe 25 ya mwezi Juni, ametoa wito kwa mataifa, serikali na jamii kwa ujumla kuwapa heshima wanayositahili mabaharia kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi ya kishujaa ambayo haikuwa imepewa uzito wa kutosha. Bwana Guterres amesema nyakati hizi za COVID-19 zimeonesha wazi ni kwa namna gani kazi ya ubaharia ni ya muhimu kwa mabaharia waliendelea kuchapa kazi wakati wote pamoja na changamoto mbalimbali. Je, mabahari wanaipokeaje hatua hii? Hilda Phoya wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam amezungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha mabaharia Tanzania na ametaundalia makala ifuatayo.  

 

Audio Credit
Loise Wairimu/Hilda Phoya
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
IMO