Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimi kama mbunge ni wajibu wangu kuielimisha jamii jinsi ya kujikinga na COVID-19-Mbunge David Karubanga wa Uganda

Mimi kama mbunge ni wajibu wangu kuielimisha jamii jinsi ya kujikinga na COVID-19-Mbunge David Karubanga wa Uganda

Pakua

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo mchango muhimu wa mabunge na wabunge unatambuliwa katika kuwawakilisha wananchi na kupaza sauti zao ili serikali imweke mwanajamii katika katika vipaumbele vyake inapoweka mipango ya nchi. Katika zama hizi za COVID-19, mabunge na taasisi nyingine za serikali nazo zimelazimika kwa kiasi fulani kufuata utaratibu mpya kujikinga na virusi ikiwemo kuweka umbali kati ya mtu na mtu na hata wakati mwingine kulazimika kufanya kazi nje ya majengo ya bunge kama ilivyo kawaida. Lakini je katika nyakati hizi ambazo mchango wao unahitajika zaidi, wamefanya nini kuwaelimisha wananchi dhidi ya virusi vya corona? Kupitia mahojiano haya na John Kibego, Mbunge David Karubanga wa Kaunti ya Kigorobya nchini Uganda anaeleza hatua alizozichukua kwa jamii yake anayoiwakilisha.

Audio Credit
Loise Wairimu/John Kibego
Audio Duration
3'39"
Photo Credit
UN Women /Aidah Nanyonjo