Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Women/Carlos Rivera

Wanawake Afrika Mashariki waleta maendeleo katik jamii husika

Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake duniani masuala mengi yameangaziwa, ikiwemo umuhimu wa kumwezesha mwanamke lakini suala ambalo ni la msingi na wakati mwingine halimulikwi ni mchango wa wanawake wenyewe katika kujikwamua na hata kuikwamua jamii kupitia shughuli wanazozifanya.

Ni kwa kuzingatia hilo ambapo leo tunamulika wanawake watatu kutoka nchi za Afrika Mashariki. Licha ya kuwa wametoka nchi tofauti lakini wanawake hawa wamejizatiti kuboresha sio tu maisha yao bali pia kuinua jamii zao kwa ujumla kwa kutumia mbinu mbalimbali. 

Sauti
5'9"
UNICEF/Tanya Bindra

Mwanamke ajikwamua kwa juhudi zinazojali mazingira, Uganda

Wakati ulimwenguni kukishuhudiwa mabadiliko ya tabianchi na athari zake Umoja wa Mataifa unahimiza nchi na watu binafsi kushiriki katika kuyalinda mazingira kwa njia mbali mbali ikiwemo kugeuza athari kuwa faida. Uchafuzi wa hewa na ukataji miti ni miongoni mwa changamoto ambazo zinajitokeza katika utunzaji wa mazingira. Lakini nchini Uganda baadhi ya watu wameanza kupata mwamko na kutambua kuwa wasipohifadhi mazingira leo basi vizazi vya kesho viko mashakani. Miongoni mwao ni mwanamke mmoja aliyeamua kutumia nishati mbadal ambayo inajali mazingira, kulikoni?

Sauti
3'48"
World Bank/Simone D. McCourtie

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kujiendeleza

Mchango wa vijana katika kusongesha ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ni dhahiri. Ni kwa kutambua hilo ndio maana Umoja wa Mataifa  kupitia mashirika yake mbalimbali na wadau unaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika maenedeleo ya kijamii.  Nchini Tanzania vijana wameitikia wito huo  na kuchukua hatua na miongoni mwao ni Paschal Masalu  ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa liitwalo ElimikaWikiendi ambalo linawahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kujiendeleza. B

Sauti
4'18"
FIB/MONUSCO

Ninapoona wanawake wana amani hiyo inanipa hamasa kuendelea kuwasaidia- Private Deborah

Umoja wa Mataifa  umekuwa kila uchao  ukipaza sauti kuhusu umuhimu wa uwepo wa walinda amani wanawake kwenye vikosi vya ulinzi wa amani vya chombo hicho. Tangu mwaka jana Umoja wa Mataifa uliweka bayana kuwa uwepo wa wanawake kwenye vikosi hivyo una mchango mkubwa katika siyo tu kufanikisha majukumu ya ulinzi wa amani bali pia kuwezesha wanawake walio kwenye mizozo kuwa wazi na wanawake wenzao katika kuwaeleza changamoto wanazokabiliana nazo na pia kufundishwa stadi za kujikwamua kimaisha.

Sauti
4'
© UNHCR/Diana Diaz

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa vitendo.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje. Nchini Tanzania, moja ya mataifa yaliyoridhia malengo hayo, jeshi la wananchi, JWTZ limeitikia wito huo kupitia shule ambazo inazimiliki. Luteni Kanali Semunyu wa JWTZ alishiriki kikao kilichosheheni maofisa wa ngazi mbalimbali za kijeshi pamoja na wale wanaoongoza taasisi za elimu zilizoko chini ya JWTZ.

Sauti
4'53"