Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shanga zetu kutoka kaunti ya Samburu zinauzwa Marekani- Sevirina

Shanga zetu kutoka kaunti ya Samburu zinauzwa Marekani- Sevirina

Pakua

Wanawake wa jamii za asili kwa kawaida wanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kutengwa kwa muda mrefu au hata wakati mwingine mila kandamizi. Moja ya mila ambazo zinawakandamiza wanawake wa jamii hizo ni suala la umiliki wa mali ambako kwa mujibu wa mmoja wa wanawake kutoka jamii za watu wa asili ya wasamburu kaunti ya Samburu nchini Kenya wanawake hawaruhusiwi kumiliki idadi sawa ya ng’ombe na wanaume, hali hii pamoja na mabadiliko ya tabianchi vinaathiri fursa zao za vipato lakini kuna nuru kufuatia juhudi mahusis zinazolenga kuinua kipato chao kupitia kuwawezesha wanawake wanaotengeneza shanga. Kwa mujibu wa mmoja wa wanawake wanaohudhuria mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW63, jijini New York, Marekani shanga za wanawake kutoka jamii za watu wa asili na hususan kaunti ya Samburu zinauzwa Marekani, kulikoni? Ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.

Audio Credit
Arnold Kayanda/ Grace Kaneiya/ Sevirina Sangurikuri
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi