Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kampeni ya 'Mimi pia ni mhamiaji', Afrika Kusini: IOM

Nchini Afrika kusini, Shirika la Uhamiaji la kimataifa, IOM kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaanzisha kampeni iitwayo, Mimi pia ni mhamiaji yenye lengo la kuhamasisha raia wa nchi hiyo wafahamu kuwa wahamiaji nao pia ni sehemu ya jamii yao na hivyo kuleta utangamano miongoni mwa wakazi wote.

Kampeni hiyo itaendelea hadi tarehe 18 mwezi ujao ambayo ni siku ya kimataifa ya wahamiaji, ikijikita zaidi kuelimisha kuwa kimsingi raia wote wa Afrika Kusini ni wahamiaji au wana uhusiano na wahamiaji.

Kongamano la utalii barani Afrika laanza nchini Tanzania

Wataalamu wa masuala ya utalii barani afrika leo wanaanza kongamano la siku tano nchini Tanzania ambalo pamoja na mambo mengine linatazamiwa kujadilia usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi za taifa.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii linahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 kutoka barani afrika na nje ya bara hilo.

Kutoka DSM, Mwandishi wetu George Njogopa ameaandaa taarifa ifuatayo.

Gurudumu la mabadiliko Somalia halirudi tena nyuma: Balozi Mahiga

Nchi ya Somalia imepongezwa na viongozi kadha wa kadha, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, kutokana na jitihada ambazo imepiga kwenye mabadiliko ya kisiasa.

Katika hali hiyo, viongozi hawa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuiunga mkono Somalia, kwani bado inakabiliwa na changamoto za kibinadamu na za kiusalama. Tangu kuteuliwa kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Augustine Mahiga amefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba Somalia imefikia kwenye nafasi iliyoifikia sasa.

Mshindi wa hotuba ya Katibu Mkuu kutoka Kenya ataka vijana wawe na usemi zaidi

Wallace Chwala, mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, ni mmoja wa washindi wa uandishi wa mfano wa hotuba ambayo ingetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wakati wa kufungua kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Shindano hilo la uandishi wa hotuba ya Katibu Mkuu, liliandaliwa na Taasisi ya Brookins kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na ikawashirikisha vijana kutoka kote duniani. Washindi walialikwa mjini New York kukutana na Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon kwenye Siku ya Kimataifa ya Amani.

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2012

Je, wewe ni kijana ambaye amehitimu na shahada ya digrii, na unaongea lugha ya Kiingereza au Kifaransa sanifu? Je, ungependa kufanya kazi na Umoja wa Mataifa? Mtihani wa vijana waliobobea kitaaluma, na ambao wangependa kujiunga na Umoja wa Mataifa kwa mpango wa vijana waliobobea, yaani YPP, utafanyika Disemba 12, 2012.

Kuna nafasi katika idara kadha wa kadha za Umoja wa Mataifa, ikiwemo idara ya habari, ambako watayarishaji wa vipindi wanahitajika katika lugha za Kireno na Kiswahili.