Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gurudumu la mabadiliko Somalia halirudi tena nyuma: Balozi Mahiga

Gurudumu la mabadiliko Somalia halirudi tena nyuma: Balozi Mahiga

Pakua

Nchi ya Somalia imepongezwa na viongozi kadha wa kadha, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, kutokana na jitihada ambazo imepiga kwenye mabadiliko ya kisiasa.

Katika hali hiyo, viongozi hawa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuiunga mkono Somalia, kwani bado inakabiliwa na changamoto za kibinadamu na za kiusalama. Tangu kuteuliwa kama Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Augustine Mahiga amefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba Somalia imefikia kwenye nafasi iliyoifikia sasa.

Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa leo mjini New York, Joshua Mmali amemuuliza kwanza Balozi Mahiga ni ujumbe gani alouleta kwenye kikao cha 67 cha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

(PKG YA MAHIGA )