WHO: Msizike marehemu wa majanga kwenye makaburi ya halaiki
Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwa kutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi.
Kuzika marehemu ni ibada, ni heshima na kubwa zaidi husaidia wafiwa kuponya nafsi zao kwa kufunga ukurasa wa mpendwa wao wakibaki na matumaini kuwa wamempumzisha katika nyumba yake ya milele.