Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 SEPTEMBA 2023

12 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani leo inatupeleka nchini Kenya kupata tathmini ya wanamazingira kufuatia kumalizika kwa mkutano wa siku tatu wa viongozi wa Afrika kuhusu tabianchi, mkutano uliotamatishwa kwa kupitishwa kwa azimio la Nairobi ambalo lilikuwa na vipengele 10 vya hatua za kuchukua ikiwemo wito kwa viongozi wa dunia kutambua kuwa uwepo wa shughuli za kiuchumi zitoazo kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, ni fursa pia ya kuchangia katika usawa na ustawi wa watu wote duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwema za WHO na WMO. Mashinani tunakupeleka nchini nchini Sudan Kusini kusikia simulizi ya mkimbizi kutoka nchini Sudan.

  1. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Mgonjwa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt. Tedros Ghebreyesus ameuambia Mkutano wa Kimataifa wa WHO mjini Geneva, Uswisi kuwa ushahidi unaonesha kwamba mitazamo ambayo wagonjwa na familia zao huleta husababisha huduma bora, uzoefu bora wa wagonjwa, na matokeo bora.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeeleza kuwa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa kupindukia siku mbili zilizopita nchini Libya yamesisitiza haja ya kampeni ya kimataifa ya Maonyo ya Mapema kwa Wote iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres mapema mwaka jana.   
  3. Na Leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limezindua miongozo miwili iliyoundwa ili kuimarisha juhudi za kuzuia watu kujiua. Mmoja ni muongozo ulioboreshwa kwa ajili wataalamu wa vyombo vya habari na pili Muhtasari wa sera kuhusu vipengele vya afya vya kuyafanya majaribio ya kujiua na kujiua yasiwe jinai.
  4. Na mashinani leo Aziza Harba Idriss, mkimbizi kutoka Sudan ambaye alikimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini kupitia njia hatarishi akisaka usalama anasimulia changamoto alizozipitia.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'45"