Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 SEPTEMBA 2023

05 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina ikimulika Siku ya kimataifa ya hisani  au kuwaonea huruma wagonjwa na maskini. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo yanayojiri katika mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi nchini Kenya na ujumbe wa Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi akitamatisha awamu yake hii leo. Katika mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?

  1. Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi ukiingia siku ya pili hii leo huko Nairobi, Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bara la Afrika lina asilimia 30 ya akiba ya madini ambayo ni muhimu katika kuzalisha nishati jadidifu na teknolojia zinazotoa kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, rasilimali ambazo zinaweza kuifanya Afrika kuwa kitovu cha nishati jadidifu duniani iwapo zitatumika kiuendelevu na kwa haki.
  2. Tukisalia kwenye mkutano huo, mmoja wa washiriki ni Dkt. Victor Yamo kutoka shirika la World Animal Protection la kulinda haki za wanyama na anasisitizia umuhimu wa kuwa na mifumo endelevu ya ufugaji.   
  3. Na Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi ametamatisha awamu yake hii leo kwa kuwaeleza wajumbe kuwa mivutano ya kisiasa katu  haiwezi kuisha duniani, lakini mivutano hiyo ipatiwe suluhu si kwa mmoja kushinda na mwingine kupoteza bali kwa kuridhiana kupitia maazimio yanayopitishwa na Baraza hilo.
  4. Na mashinani tutakupeleka nchini Jamhuri ya Kiemokrasia ya Congo, DRC ambapo mizozo na ongezeko la idadi ya watu wanaokimbia makazi yao mashariki mwa nchi hiyo linawafanya watoto kuingia katika janga kubwa la kipindupindu kuwahi tokea tangu mwaka 2017”.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
16'23"